25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mbwa wa polisi Hispania kuchezewa muziki

JOSEPH HIZA NA MITANDAO        |     


MAKAZI nchini Hispania yamepitia ukarabati uliochukua miezi mitatu, ambao ulihusisha uwekaji dari mpya, vyumba vya kifahari, viyoyozi mfumo wa kupasha joto na muziki.

Unaweza kudhani mabadiliko yote haya ya katika hoteli ya nyota tano au hekalu la kifahari, lakini ukweli ni kwamba ukarabati huo mkubwa wa gharama unafanyika katika makazi ya mbwa wa polisi wa Jiji la Madrid nchini Hipania.

Lengo la mabadiliko ya mazingira hayo, ambayo yamekamilika mapema mwaka huu ni kuboresha mazingira ya kazi ya mbwa polisi hao.

Mfumo malumu unaotoa muziki uliowekwa na Polisi wa Manispaa Kuu ya Hispania unalenga kuwaliwaza mbwa hao wanaotoa huduma ya usalama katika manispaa hiyo.

Manispaa inamatumaini kwamba mfumo huo mpya utapunguza viwango vya msongo wa mawazo ambao unawapata mbwa.

Mfumo huo unaotoa muziki wa aina ya classic mara kadhaa kwa siku unaofahamika kama ‘Mozart effect.’

Mbwa hao 22 wanafanya kazi ya upelelezi katika nyanja tofauti katika kikosi cha polisi wa manispaa hiyo.

Baraza hilo la Madrid, ambalo linaangazia masuala ya walinzi hao, limesema mbwa hao hukumbana na viwango vikubwa vya msongo wa mawazo kutokana na kazi yao.

Vifaa hivyo vimewekwa kama njia ya kuboresha sehemu ambazo mbwa hao wanaishi.

Mbwa katika kitengo hicho wana utaalamu wa kuchunguza milipuko au dawa za kulevya na husaidia katika shughuli za uokozi yanapotokea majanga na ajali.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la tabia za wanyama-Veterinary Behavior mwaka 2012 ulibainisha kuwa muziki aina ya classic una uwezo wa kuwasaidia mbwa kupunguza wasiwasi.

Sajenti wa polisi, Rafael de la Gándara, anayeoongoza kitengo hicho amesema uboreshaji wa makazi ya mbwa utawasaidia kuimarisha hali zao za maisha na kazi wanayoifanya.

Alisema mbwa hao wanahitaji mapumziko na kuchangamshwa ili wawe macho na waweze kufuata maagizo ya kamanda wanapokuwa kazini na kutekeleza wajibu wao wanapohitajiwa kwa kazi ya dharura.

”Mfano, endapo mbwa anatafuta dawa za kulevya, huchimba chini ardhini, kwa kweli si jambo jema iwapo anatafuta mabomu,” alisisitiza Sajenti de la Gándara.

Uboreshaji wa makazi yao pia ulijumuisha kuwekwa kwa viyoyozi kuhakikisha hawaathiriwi na jua linaloambatana na joto wakati wa majira ya joto na kuwalinda na baridi nyakati za majira ya baridi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles