Wanawake 12 waliojifungua uzeeni

0
1497
 1. Daljinder Kaur

MKAZI huyu wa Amritsar Jimbo la Punjab, Kaskazini mwa India kwa sasa anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke mzee zaidi kuwahi kuzaa duniani.

Alikuwa na umri wa miaka 72 na mumewe 79 wakati mtoto wao wa kiume alipozaliwa Aprili 19, 2016. Ni ngumu kukutana na wenzi majasiri kama hao katika dunia hii kwa uthubutu wa kitendo hicho.

 1. Omkari Panwar

Kutokana na dhamira yao ya kuhakikisha anampatia mumewe mrithi wa mali yao, Omkari alilazimika kupitia tiba ya kumwezesha kushika mimba. Kutokana na sababu hiyo, alijifungua mapacha – mvulana na msichana huko Muzaffarnagar, Uttar Pradesh kwa njia ya kisu Juni 27, 2008 akiwa na umri wa miaka 70.

 1. Rajo Devi Lohan

Mwanamke huyu wa India alijifungua mtoto wake wa mwisho wakati akiwa na umri wa miaka 69. Kwa muda mrefu alikuwa akichukuliwa kuwa mama mzee zaidi kurekodiwa duniani katika historia ya utabibu. Mtoto huyo hadi sasa ana afya njema.

 1. Elizabeth Adeney

Ni mama mzee zaidi nchini Uingereza ambaye katika umri wa miaka 66 alijifungua mtoto. Mama huyo alikuwa katika hali nzuri kiafya na mtoto hakuwa na tatizo lolote. Elizabeth kwa sasa ni mzungumzaji mwalikwa wa  mara kwa mara katika vipindi vya televisheni na redio.

 1. Bhateri Devi Singh

Mwanamke huyu mwingine wa India katika umri wa miaka 66, alikuwa mama wa watoto watatu mapacha! Watoto wote hao watatu walikua vizuri kama kawaida. Cha kushangaza zaidi mama huyu bado ana afya nzuri.

 1. Adriana Iliescu

Mwanamke mwingine, ambaye dunia inapaswa kujivunia ni raia wa Romania. Katika umri wa miaka 66 dunia ilikuwa ikisubiri kushuhudia ujio wa mapacha watatu, lakini ni mmoja tu aliyeweza kuishi. Mtoto huyo kwa sasa ndiye binti kipenzi kuliko wote nchini Romania.

 1. Maria del Carmen Bousada de Lara

Mwanamke huyu wa Hispania aliwadanganya madaktari kwa kuwaambia kwamba alikuwa na umri wa miaka 55. Baada ya ukweli kufichua kuwa alikuwa na miaka 66, hakukuwa na lolote la kufanya kurekebisha hali. Akajifungua watoto wawili, lakini akafariki dunia miaka isiyozidi mitatu baadaye.

8. Valentyna Pidverbna

Mwanamke huyu wa Ukraine katika umri wa miaka 66 alijifungua mtoto wake wa kwanza na wa pekee. Kwa kufahamu kiwango cha huduma za afya ukanda wa Ulaya Mashariki, usingeweza kuamini kuwa angeweza kuhimili changamoto aliyopitia kitabibu.

 1. Annegret Raunigk

Mwanamke wa Ujerumani alikuwa na umri wa miaka 65 wakati alipojifungua watoto wanne. Kwa ujumla, alikuwa na watoto 17 wenye umri hadi miaka 44! Ni mwanamke pekee wa Ulaya mwenye umri zaidi ya 60 kuwa na watoto wengi.

 1. Memnune Tiryaki

Mwanamke huyu wa India alizaa mtoto wake wakati akiwa na umri wa miaka 62. Awali alijaribu kutafuta mtoto kwa miaka 35 bila mafanikio.

Lakini katika umri wa kupokea pensheni, aliweza kufanikisha ndoto yake shukrani kwa ujio wa tiba za kisasa

 1. Dawn Brooke

Mwanamke wa Kiingereza katika umri wa miaka 59, alijifungua kwa njia ya kawaida. Amerekodiwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia Guinness World Record Book kama mwanamke mzee zaidi kujifungua mtoto kwa njia ya asili.

 1. Raisa Akhmadeeva

Mwanamke wa Urusi katika umri wa miaka 56, alijifungua mtoto kwa njia ya asili. Alikuwa mtoto wake wa kwanza na hakulazimisha kupitia tiba maalumu. Mtoto alizaliwa mapema na miaka miwili ya kwanza walihaha kuhakikisha anaishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here