24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AWATANGAZIA VITA WATAKAOFILISI SACCOS

Na Mwandishi Wetu, Rufiji


mohamed-mchengerwaMBUNGE wa Rufiji mkoani Pwani, Mohamed Mchengerwa (CCM) ametangaza kwamba atapambana na ufisadi kwenye vikundi vya kuweka na kukopa (Saccos) jimboni kwake kuhakikisha hakuna anayetafuta fedha hizo wakati mamia ya wananchi wakiambulia patupu.

Mchengerwa alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Vicoba endelevu vinavyojumuisha vikundi tisa vyenye akiba ya zaidi ya Sh milioni 45.

Alisema licha ya wananchi kujiunga katika vikundi kwa nia ya kusaidiana, wapo wachache wanatumia makundi hayo kutapeli.

“Wapo wanaofanya ufisadi ili kuua vikundi…,  nitashughulika nao wote kama ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli anayepinga ufisadi hata kuanzisha mahakama ya mafisadi,” alisema.

Mchengerwa ambaye alichangia Sh milioni 6.5 katika uzinduzi huo, aliwataka wana vikundi hao kuhakikisha fedha hizo zinatumika katika maendeleo na kuonya wenye mtindo wa kugawana fedha zinapotolewa.

‘’Naomba fedha hizi zitumike katika matumizi sahihi, nakumbuka hivi karibuni nilitoa pikipiki katika vikundi lakini taarifa zilizopo ni kwamba watu wameenda kuuza na kugawana fedha jambo ambalo si sahihi,tunajirudisha nyuma wenyewe,’’alisema Mchengerwa.

Alisema wananchi wa Rufiji ni masikini na wapo nyuma katika maendeleo hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele kuukataa umasikini huo kwa vitendo.

‘’Nimejitolea kusaidia watu wa Rufiji kwa kuwa mlinichagua  niwawakilishe.

“Naombeni kila mmoja aguswe na umasikini tulionao na awe na dhamira ya dhati ya kuutokomeza.

“Vikundi hivyo vitumike vizuri mkopeshane muweze kuendesha na kuanzisha biashara zenu,naahidi kuwa bega kwa bega na nyie na leo hii (juzi) nawakabidhi mke wangu Farida Mchengerwa kuwa mlezi wenu ili msaidiane,’’alisema Mchengerwa.

Mlezi wa vikundi hivyo, Farida Mchengerwa,aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kujiunga na vikundi hivyo waweze kukopesheka kwa sababu  inajulikana kuwa masikini hakopesheki kutokana na masharti yanayowekwa na taasisi za fedha ambayo wengi hawana uwezo wa kuyamudu.

Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi hivyo,Abdulrahman Hafidh,alisema vikundi hivyo kwa sasa vina wanachama zaidi ya 220.

Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa wanavikundi kuhusu Vicoba endelevu jambo ambalo Mchengerwa aliahidi kulishughulikia kwa kumuwezesha mwalimu   aendelee kuwapa elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles