24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Azam Media yazindua tamthilia mpya ya Mzani wa Mapenzi     

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Azam Media LTD kupitia Chaneli ya Sinema Zetu HD namba 106 imezindua tamthilia mpya iitwayo Mzani wa Mapenzi, inayowahusisha wasanii maarufu Irene Uwoya na Patcho Mwamba.

Tamthilia hii imezinduliwa jana katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Msimamizi Mkuu wa Sinema Zetu, Sophia Mgaza, alieleza kuwa Mzani wa Mapenzi ni tamthilia inayovutia kwa namna inavyoonesha maisha katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, pamoja na vivutio vya kitalii vilivyopo katika ufuo wa Bahari ya Hindi.

Mgaza amesema kuwa tamthilia hii inamleta Irene Uwoya na Patcho Mwamba kwenye sura mpya baada ya ukimya wao, na inawaleta pamoja katika hadithi yenye mvuto inayowalenga wanandoa wenye mitazamo tofauti juu ya furaha na thamani ya ndoa. Kwa upande mmoja, Cecy anaamini kuwa ndoa ni tunu inayopaswa kulindwa, huku mumewe Victor akiona kuwa kuwa na mpango wa kando ni kipimo cha ubabe wake katika ndoa.

Tamthilia hii imejumuisha waigizaji wengi maarufu na chipukizi kama Marium Ismail (Cecy), Sharon Kabwita (Kai), Irene Uwoya (Cleopatra), Habibu Mtambo (Victor), Alex Mgeta (Alex), Marium Fereji (Mercy), Lightness Lodvick (Peace), Patcho Mwamba (Bruno), na Fredy Kiluswa (Dr. Maja).

Mzani wa Mapenzi itaanza kuonyeshwa tarehe 23 Agosti 2024 kwenye Chaneli ya Sinema Zetu HD namba 106 kila Ijumaa hadi Jumapili saa moja usiku, kuchukua nafasi ya tamthilia ya Toboatoboa itakayomalizika Agosti 18, 2024.

Mgaza aliongeza kuwa lengo la Azam Media LTD ni kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji wake na kusukuma sanaa ya Tanzania kimataifa, hususan katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na maeneo mengine yanayofikiwa na AzamTVMax.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles