29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanariadha achomwa moto na mpenzi wa zamani

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei,mwenye umri wa miaka 33, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Kenya baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake wa zamani(Ex).

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa na vyombo vya habari nchini Kenya, mwariadha huyo ameungua zaidi ya 75% ya mwili wake.

Idaiwa kuwa shambulio hilo lilitokea nyumbani kwake magharibi mwa Kenya, ambako alikuwa akifanya mazoezi.

Aidha polisi wanasema mwanaume huyo anayeitwa Dickson Marangach, naye pia alijeruhiwa kutokana na miale ya moto.

Ripoti iliyowasilishwa na msimamizi wa Kaunti hiyo imesema kuwa wawili hao walikuwa wakizozana kuhusu kipande cha ardhi ambacho kiko karibu na mpaka wa Uganda ambacho Cheptegei alitaka kununua na kujenga nyumba ili kuwa karibu na vituo vingi vya mafunzo ya riadha nchini Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles