22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

DK. SHEIN AWAHAKIKISHIA WANANCHI HUDUMA HOSPITALINI

Na MASANJA MBAULA- PEMBA


 

dk-ally-mohamed-sheinRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindunzi, Dk. Ally Mohamed Shein  amesisitiza kuwa huduma za vipimo vya CT Scan na X-ray  pamoja na huduma za mama na mtoto zitaendelea kutolewa bure katika Hospitali za Mnazi Mmoja  na  Abdalla Mzee mkoani pemba.

Alisema kutolewa bure kwa vipimo hivyo ni utekelezaji wa ilani ya  uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015  – 2020.

Dk. Shein ameyaeeleza hayo   mkoani pemba wakati akifungua Hospitali ya Abdalla Mzee ambayo imejengwa upya kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China.

Alisema kwamba ili kufanikisha azma hiyo serikali imejipanga kupeleka madaktari bingwa na wataalamu wa kutosha katika hospitali hiyo ambao watashirikiana kutoa huduma kwa wananchi.

“Nasisitiza kwamba huduma za mama na mtoto zitaendelea kutolewa bila ya malipo katika hospitali zote za Unguja na Pemba,” alisema.

Alisema lengo la kuipatia vifaa Hospitali ya Abdalla Mzee na kuifanya kutoa huduma bora, sawa na hospitali ya Mnazi mmoja na hivyo kuwapunguzia gharama  wananchi kwa kufuata huduma  hizo hospitali za Unguja.Aliwataka madakatari na wahudumu wa  afya kuwa waadilifu na kufuata maadili ya taaluma yao na kutumia lugha vizuri na hekima wakati wa kuwahudumia wagonjwa.
“Nawasisitiza sana madaktari na wahudumu katika hospitali hii tumeifungua ikiwa na vifaa vya kisasa ni budi kufuata maadili na kutumia lugha za hekima na busara kwa wananchi wakati wanapokuja kufuata huduma,” alisema.

Alisema Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mohamedd Thabit Kombo amesema kukamilika hospitali hiyo  na kuwepo wafanyakazi katika hospitali hiyo ni kuongeza huduma za afya kwa wananchi kama ilivyo ilani ya uchaguzi ya zanzibar.

Waziri ameipongeza Serikali ya China kwa misaada yake  kwa zanzibar na kuahidi kuendelea kuithamini kudumisha undugu na uhusiano uliopo baina ya watu wa China na Zanzibar.

balozi wa China   nchin, i Dk. LU Youqing alisema wataendeleza  kuisaidia Zanzibar katika nyanja mbalimbali ikiwamo elimu,afya na michezo.

Pia ameahidi kuendelea kuleta madaktari bingwa ambao watafanya kazi katika hospitali hiyo na kuwapa mafunzo madaktari wazalendo waweze kuvitumia vifaa vya kisasa ambavyo vimewekwa katika hospitali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles