24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

TUTARAJIE KUMUONA MESSI WA KARATASI ENGLAND

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


messMSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, ni miongoni mwa wachezaji bora duniani kwa sasa na bora kwa kipindi chote.

Mashabiki wengi wa soka duniani, hupenda kumshindanisha na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo,  hata hivyo  hawajatofautiana sana.

Lakini kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amepata shauku iwapo klabu za Ligi Kuu England (EPL), zitaweza  kuwasajili nyota hao bora duniani kutoka Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, kabla hawajafika mwisho wa uwezo wao wa kusakata soka uwanjani.

Kikosi  cha Pochettino, kilimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita wakipoteza nafasi ya kutwaa taji hilo katika michezo ya mwisho ya ligi hiyo.

Pochettino anaeleza kuwa Ronaldo yupo tofauti kidogo na Messi kutokana na kuwahi  kucheza Ligi Kuu bora ulimwenguni ya England, ambapo Messi hakuwahi kufanya hivyo.

Wachambuzi wa soka duniani wanadai kuwa Ligi Kuu England (EPL) ndiyo ligi ngumu kuwahi kutokea ambayo inahitaji mchezaji kuwa na  nguvu na kasi ya ajabu.

Hata hivyo, klabu za EPL zinaonekana kutokuwa na uwezo wa kuwasajili wachezaji hao wawili.

Kwa sasa klabu ya Manchester City imetajwa kuwa mbioni kuinasa saini ya Messi, Pochettino haoni kama jambo hilo linawezekana, licha ya kuamini kuwa  iwapo klabu hiyo itaamua kufanya hivyo huenda nyota huyo akatua katika viwanja vya Etihad dirisha dogo la usaji mwakani.

Akihojiwa na mtandao wa Marca, kocha huyo alieleza: “Wachezaji hawa ni adimu kupatikana katika timu, Real Madrid na Barcelona tayari wana hawa wachezaji, ni nani atawapokonya, ni jambo gumu sana.

“Lakini, kama klabu ikiwa na nguvu ya fedha tutawashuhudia Messi au Ronaldo wapya England, vipaji hivyo vinaweza kuwa hapa England muda wowote.”

Lakini bado kuna maswali mengi kwa wachezaji ambao hupenda kupata rangi ya mpira kama ilivyo kwa Messi, iwapo atamudu na kuendelea  kuwa bora na kushinda mabao 169 katika michezo 214 atakapokuwa EPL kama ilivyo La Liga.

Wengi watakumbuka namna Chelsea walivyoweza kuwafunga Barcelona katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, misimu mitatu iliyopita.

Katika mchezo huo Messi alitolewa nje, alikuwa nje ya uwanja kiakili na kila mtu akimwona kuwa tofauti kwa kushindwa kuwa hata nusu ya ubora wake.

Hali hiyo ilitokana na usumbufu uliofanywa na wachezaji wa Chelsea ambao hawakumruhusu Messi kumiliki mpira hata mara moja.

Hata hivyo, hiyo haimaanishi kwamba Messi hataweza kufanya vizuri wakati akiwa EPL, kutokana na sababu hizo.

Ni ukweli kwamba hilo ni jambo dogo sana kwa Messi ili kumzuia asifanye yake uwanjani, kutokana na uwezo wake inahitaji mbinu ya ziada.

Mara  ya mwisho kwa Ronaldo kuwa England, aliondoka akiwa nafasi ya tatu ya mchezaji bora Ulaya, Ballon d’Or mwaka 2008, wakati huo Fernando Torres akiwa miongoni mwa waliokuwa wakifanya vizuri katika tuzo hiyo wakati huo akicheza Liverpool.

Hiyo ilikuwa miaka nane iliyopita, ambapo kwa sasa inakaribia tisa tangu England ijipambanue kuwa ni ligi bora Ulaya kwa kuweza kumnyakua mchezaji bora duniani.

Lakini kwa ujio wa makocha bora ulimwenguni, mwaka uliopita au ujio wa Jurgen Klopp, Pep Guardiola na Antonio Conte, muungano huo umeleta sifa ya ziada katika ligi hiyo.

Hivyo kuwa na uwezo wa kuvutia wachezaji wenye vipaji ambao wanaweza kuwa tayari kujiunga na klabu za England kutokana na ubora uliopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles