23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ACT-WAZALENDO YAMLILIA FIDEL CASTRO

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


 

fidel-castroCHAMA cha ACT Wazalendo kimetuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Cuba, Raul Castro kutokana na kifo cha kaka yake ambaye aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Fidel Castro, kilichotokea juzi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa   Dar es Salaam jana na Katibu wa Kamati ya Nje ya ACT Wazalendo, John Mbozu, ilisema   maisha ya Castro hayakuwa manufaa kwa Wacuba  pekee bali kwa dunia nzima hasa nchi zinazoendelea.

“Alikuwa ni mmoja ya miamba imara ya mapinduzi ya karne ya 20 kupitia mapinduzi ya ujamaa ya Cuba na ameacha alama ya kudumu katika maisha ya WaCuba na darasa maridhawa kwa nchi zinazoendelea kuweka msisitizo juu ya umuhimu wa ujamaa kwa dunia.

“Pia  licha ya utitiri wa vikwazo kutoka nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani, Cuba iliweza kufuta ujinga kwa asilimia 99 na ni moja ya nchi zenye mfumo bora wa afya hasa kwa kusomesha madaktari wingi zaidi duniani,” alisema Mbozu.

Alisema Cuba imekuwa ikitoa msaada wa madaktari kwa nchi za Amerika ya Kusini, Afrika na Asia hadi kuvuka kiwango kilichowekwa na nchi zote za G8 ikiwa na ukuaji wa uchumi unaokwenda sambamba na maendeleo ya watu wengi.

Mbonzu alisema Castro alifungamana moja kwa moja na Afrika kwa kusaidia harakati za ukombozi wa bara hilo kutoka katika makucha ya Ukoloni na Ubeberu ambazo zilikuwa na makao makuu yake nchini.

“Afrika itamkumbuka Castro kwa mchango mkubwa ambao ambao nchi yake iliutoa katika kufanikisha harakati za kudai uhuru kwenye nchi mbalimbali za barani Afika kama, Afrika ya Kusini, Namibia, Angola, Msumbiji na Kongo,” alisema Mbonzu.

Alisema Cuba imepoteza kiongozi wake, Afrika imepoteza rafiki wa kweli, Tanzania imepoteza mshirika katika ukombozi wa Afrika na ACT Wazalendo imepoteza mjamaa mwenzao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles