27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WANA NDOA WAUANA UKWENI

Na KADAMA MALUNDE-SHINYANGA


 

kamanda-wa-polisi-mkoa-wa-shinyangaMWANAMUME mmoja, Kadami  Mwendagiza (34), amemuua mkewe, Mwajuma Jange (29) kwa kumkaba shingo na yeye akajinyonga kwa   kanga katika tukio lililotokea katika Kijiji cha Ishinabulandi Kata ya Samuye wilayani Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,  Muliro Muliro, tukio hilo lilitokea Novemba 25, mwaka huu, saa 3:30 asubuhi.

Alisema Mwendagiza mkazi wa Kijiji cha Bugimbagu   alimuua mke wake kwa kumkaba shingo na kusababisha mauti yake baada ya kukosa hewa.

Muliro alisema baada ya mwanamume huyo kumuua mkewe naye alijiua kwa kujinyonga kwa   khanga na kujitundika katika kenchi ya chumba walimokuwa wanaishi wanandoa hao.

“Kabla ya tukio wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa familia wa muda mrefu hali iliyosababisha wanandoa hao waondoke Dar es salaam walipokuwa wanaishi na kufikia kwa wazazi wa mwanamke katika Kijiji cha Ishinabulandi kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro wao,” alisema kamanda Muliro.

Alisema siku ya tukio, wanandoa hawa waliamka salama na wazazi wa mwanamke waliwaacha nyumbani kwenda kwenye shughuli zao za uchumi lakini baadaye  ugomvi ulianza tena na ndipo yalipotokea madhara hayo.

Kamanda alisema marehemu hao wameacha mtoto mmoja, Ibrahim Kadami (10) ambaye ni  mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Bugijibaga wilayani Shinyanga.

Muliro alisema maiti zote mbili zimefanyiwa uchunguzi na ndugu wamekabidhiwa   waendelee na shughuli za mazishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles