24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KASHFA YA NGONO KITUO CHA MABASI UBUNGO

Na ESTHER GEORGE-DAR ES SALAAM


 

ubungoWANAWAKE wajasiriamali katika Kituo  Kikuu cha mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani cha Ubung0 (UBT), wamelalamikia kuombwa rushwa ya ngono na baadhi ya madereva wakiwa katika biashara zao.

Walikuwa wakizungumza na MTANZANIA   mwishoni mwa wiki katika semina ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake iliyoandaliwa na mradi wa ‘Thamani yako hailinganishwi na kitu’   Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wanawake hao, wamekuwa wakinyanyaswa kwa ngono na madereva, makondakta na mawakala wa mabasi wanapokwenda kuuza bidhaa zao katika mabasi hayo.

Mmoja wa wauza mikate katika kituo hicho, Mariam Amani, alisema wanaohusika na magari ndani ya kituo hicho wengi wao wamekuwa wakiwaomba rushwa ya ngono ili wawaruhusu kuingia katika mabasi kuuza bidhaa.

“Yaani sisi wauza mikate tunapata shida ukizingatia wanunuaji ni abiria ambao wanasafiri.

“Ukitaka kuingia kwenye basi wahusika wa gari hilo wanakuambia hakuna kuingia kuuza huku mwenzako anaingia na anauza, ukijiuliza nini chanzo… kwa sababu alikuomba ngono ukamkatalia,”alisema Mariam.

Alisema changamoto nyingine wanazokabiliana nazo wakiwa kazini ni kutolewa lugha chafu, kudharauliwa, kutomaswa miili yao bila ridhaa na kufukuzwa ovyo kwenye magari wanapoingia kuuza bidhaa.

Maria Juma, alisema changamoto kubwa anayopata ni kunyanyaswa kwa jinsia endapo akiombwa penzi akakataa.

“Wanatangaziana chakula chako kibovu na matokeo yake ni kukosa wateja,” alisema.

Mratibu wa mradi huo, Elizabeth Tendwa, aliliambia MTANZANIA kuwa kinachofanywa na watu wanaohusika na mabasi hayo ni kinyume na sheria pia rushwa ya ngono inadhalilisha utu wa watu wengine.

Alisema wanawake wanatakiwa kujengewa uwezo wa  kutambua thamani yao, kujitambua na kujithamini ikiwa ni pamoja na kusema ‘hapana rushwa ya ngono’   waweze kufikia malengo yao.

Alisema watafanya kampeni ya kupita sehemu mbalimbali katika juhudi za kukomesha ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na wasichana.

“Naamini semina hii itasaidia kupunguza magonjwa mbalimbali kama Ukimwi na yale ya zinaa,” alisema Elizabeth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles