23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge atishia kufanya vurugu kisa maji

Arodia Peter, Dodoma

Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM) ametishia kuzusha ‘vagi’ jimboni kwake kama Serikali haitawaondolea kero ya maji.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma, Kadutu amesema jimbo lake kwa muda mrefu limetengwa na halipewi kipaumbele huku wananchi wake wakitaabika kwa ukosefu wa maji.

Kadutu ambaye amezungumza kwa hisia, amesema yeye na wananchi wanakwenda kuziba Mto Malagalasi kwa sababu mradi wa Mto huo badala ya kuhudumia pia wananchi wa Ulyankulu, umeelekezwa Kaliua na Urambo mkoani Tabora.

“Mheshimiwa Waziri na wataalam mlioko hapa nyuma yangu hebu fanyeni mnavyoweza, je tutatengwa hadi lini?, sisi sio wakimbizi kama hamtaki kutupa tawala za mikoa tupeni maji, wataalam msikie tutaleta vagi hata wao hawatakanyaga huko,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles