26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE, VIONGOZI WATANO CHADEMA WAFUTIWA DHAMANA, WAWEKWA MAHABUSU

Bethsheba Wambura na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wamefutiwa dhamana na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mbowe, viongozi wengien ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Viongozi hao wameripoti kituoni hapo leo Jumanne Machi 27, saa tatu asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kuitikia wito wa polisi ambao wamekuwa wakiwahoji kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali Februari 16, mwaka huu.

Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Kihwelo wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi ya viongozi walikuwa wanakaidi kuripoti polisi kila wanapotakiwa kufanya hivyo huku Msigwa akiongezwa katika orodha ya viongozi hao baada ya kuhojiwa jana na kupewa dhamana ambayo pia leo imefutwa.

“Baada ya kuhojiwa leo, wakaambiwa waendelee na mambo mengine wamepelekewa katika Ofisi ya Mpelelezi wakavuliwa viatu na mikanda, wakawekwa mahabusu.

“Walitakiwa kupelekwa mahakamani lakini bado kuna hali ya kusuasua lakini kwa mujibu wa ZCO, wameambiwa wamewekwa mahabusu kwa sababu wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi yao walikuwa wanakaidi wito wa polisi wakitakiwa kufika polisi, lakini hiyo si sababu ya msingi kwa sababu wangeweza kuwafutia wale ambao hawapo na si hawa wanaokuja kila siku,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema ZCO amewaambia kesho watafikishwa mahakamanai lakini hadhani kwa sababu kuna mpango mbaya zaidi ila wanachokifanya leo ni kupeleka maombi Mahakama Kuu kuomba kesho wafikishwe mahakamani.

Walioshindwa kuripoti kituoni hapo Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kutokana na kufiwa na msiba huku Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akidaiwa kuwa nje ya nchi kwa matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Walawiti wa watoto Raisi anawapa msamaha.
    Mabinti wanaojazwa mimba na wanaume wazee, viongzi, Wanawekwa jela na kustopishwa kimasomo.
    Wala rushwa wakuu, Kwa vile wanavaa kijani wanaondolewa hapa na kupelekwa kule,
    Walioshindwa kutetea, kulinda mali ya umma wanakula sahani moja na Raisi kukandamiza upinzani.
    Wahusika wakuu wa madawa ya kulevya wengi ni viongozi wakuu wa chama tawala wamepewa kinga,
    Escrow ambayo imekula mabilioni ya Watanzania Raisi aliyepita alisimama hadharani na kukanusha si mali ya umma,
    Waliosaini mikataba yote mibovu ya madini, ni Maraisi wa CCM na mawaziri wake ambao bado wako madarakani.
    Elimu imeshuka sababu Viongozi wameamua kuwekeza kwao na kutumia pesa kinyume cha mipango ya maendeleo ya nchi
    Wapinzani, wengi wenye elimu safi, wapigania haki, wananyanyasika, tekwa, na wengine kupotea kabisa bila kujua ni nini kiliwasibu.
    Aquilina kapigwa risasi hadharani na polisi. hatumjui huyu polisi badala yake viongozi wapinzani Rumande na kesi nzito. Sasa Raisi wetu anaomba Maaskofu wamwombee, halafu anawageuka na kuwaita wasaliti. Katiba ambayo ni haki ya Watanzania, inawaweka maaskofu hatiani na Watanzania mnachekelea.
    Tunaulizwa na Raisi ni nani katuroga. Majibu yote yako wazi ni nani si msikivu. Anayelazimisha watu waone atendalo tu. Na Watanzania mnaounga mkono, Wasomi na wengine, mnajua ni wote ambao mnaliloga Taifa kwa kufumbia macho. Ni kwaresma, Walawiti wametolewa jela, Wapigania haki wanabuguthiwa kama kikunguni. Sala tunazowaomba Maaskofu kama tunajua tumemkosea Mungu kwa nini tusiziungame wenyewe watenda dhambi kama ni kweli tunamwogopa na Kumcha Mungu. Kwenda makanisani, kutoa michango mikubwa ili tusifiwe ndivyo makuhani waongo, mafalisayo na makadusayo ndivyo walivyofanya ili waonekane wazuri mbele za watu. Lakini mungu ndiye anayeona yote ya gizani.
    Ni hippocratic kubwa kwa kiongozi yeyote kujifanya mzuri sana na malaika mbele za Watu.Ni bora afanyaye mema gizani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles