27.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Mbaroni kwa tuhuma za kumuua shemeji yake

Ashura Kazinja, Morogoro

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma ya kumuua shemeji yake, huku watu wengine 39 wakishikiliwa kwa makosa ya uporaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi kutoka maungoni na kujeruhi katika maonesho ya nanenane mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, akizungumzia mtuhumiwa wa mauaji,  alisema chanzo cha tukio ni ugomvi wa kimapenzi kati ya mtuhumiwa na mke wake.

Alisema mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Shinje Jilangila (30) mkulima na mkazi wa Mbamba, anadaiwa kumkata kichwani shemeji yake aitwae Dotto Luhende (28) kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia kifo hapo hapo.

Alisema mtuhumiwa alienda nyumbani kwa shemeji yake kumfuata mkewe Kurwa Luhende, ambaye alikuwa ameenda kwa kaka yakekutokana na ugomvi kati yake na mumewe.

Kamanda Mutafungwa alidai kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kufika kwa shemeji yake alipewa hifadhi ya kulala ili asubuhi ya siku inayofuata kikao cha usuluhishi kifanyike.

Hata hivyo alisema ilipofika saa 6 usiku wa siku hiyo ya Agosti 12, mtuhumiwa alimuua mwenyeji wake ambaue ni kaka wa mke wake kisha kukimbia.

Alisema wananchi wakishirikiana na polisi, walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni, na anahojiwa na jeshi hilo na mara upelelezi wa awali utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Wakati huohuo jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 39 kwa makosa ya uporaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi kutoka maungoni na kujeruhi katika maeneo ya ndani na nje ya uzio wa Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya maonesho ya wakulima katika Manispaa ya Morogoro ambapo sherehe za sikukuu hiyo zilikuwa zikiendelea.

alisema watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na pikipiki moja aina ya SANLG rangi nyeusi yenye namba MC 225 BQT, mapanga 4 na visu 4 ambavyo walikuwa wakivitumia kuwapora wananchi waliokuwa wakiingia na kutoka kwenye viwanja hivyo, na kwamba watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Hata hivyo Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi hasa vijana kuacha vitendo vya utapeli, wizi, uporaji na unyang’anyi  kwani jeshi la polisi limejipanga vizuri kuhakikisha uhalifu wa aina zote unakomeshwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,679FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles