29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mhagama aagiza kemikali za kutengeneza viatu kuzalishwa nchini

Upendo Mosha, Moshi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, ameagiza wataalamu nchini, kutengezeza kemikali itakayotumika katika kiwanda cha viatu cha Karanga Moshi na kuacha kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje ili kupunguza gharama.

Mhagama aliyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Ninazo taarifa kwamba kemikali mnazotumia kama malighafi mnaziagiza kutoka nje ya nchi jambo linasababisha gharama kuwa kubwa, wakati umefika tutumie wataalamu wetu wa ndani kufanya utafiti na kuzalisha kemikali hizo kwa ajili ya kiwanda hiki na viwanda vingine pia”alisema.

Alisema, Serikali imedhamiria kuinua uchumi kutoka kuwa wa kati hadi wa kati wa juu na kuhakikisha wananchi wake wanapata ajira kupitia miradi mbalimbali inayoanzishwa nchini na kwamba suala hilo litawezekana iwapo wataalumu wataongeza ubunifu .

Mhagama pia aliagiza wabia wa kiwanda hicho ikiwemo Mfuko wa Hifadhiya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuhakikisha kiwanda hicho kinakua cha kimataifa kwa kuongeza ufanisi katika vifaa, malighafi na wataalamu wa uzalishaji wa bidhaa za ngozi nchini.

“Naupongeza mfuko wa PSSSF kwa uwekezaji katika kiwanda hiki cha viatu cha Magereza Karanga, nawashauri muwekeze kwenye maeneo yenye tija na yatakayotoa ajira na kunyanyua uchumi wa Tanzania na Watanzania kwa ujumla”alisema

Awali akizungumzia ujenzi wa mradi wa kiwanda hicho, Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, alisema kiwanda hicho ni moja ya kiwanda kikubwa Afrika Mashariki na kwamba kukamilika kwake kitagharimu zaidi ya Sh bilioni 136.

“Kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hikii kitatoa ajira kwa watu zaidi ya 3,000 za moja kwa moja lakini pia kupitia kiwanda hichi kitasaidia kukuza pato ya Mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla nategemea wananchi watusaidie kufunga mkono,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles