25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa kumtupa mtoni

Na Nyemo Malecela, Kagera

JESHI la Polisi mkoani Kagera, linamshikiria Herieth Ponsian (27) mkazi wa Kyebitembe Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za kumtupa mtoni mtoto wake na kumsababishia mauti.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema Herieth alikiri kumtupa mtoto wake, Prince Onesmo (1) katika mto wa Kanoni unaotiririsha maji machafu akiwa hai na kumsababishia mauti.

Malimi alisema Herieth anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mwanae, kosa alilolitenda Septemba 30, akiwa nyumbani kwa dada yake baada ya kutokea ugomvi na mzazi mwenzake.

“Awali Herieth alitoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali za mitaa na majirani kuwa mtoto wake amepotea na kesho yake (Oktoba Mosi mwaka huu) mtoto huyo alionekana akielea kwenye maji akiwa amefariki.

“Baada ya kukamatwa hakueleza nini kimesababisha atende ukatili huo kwa mwanae hivyo bado tunaendelea na upelelezi na kusubiri majibu ya kitabibu ya uchunguzi wa mwili wa mtoto huyo ili kujua nini chanzo cha kifo chake,” alisema.

Vilevile Malimi alisema utafiti wa kitabibu bado unaendelea ili kujua kama Herieth ana matatizo ya akili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles