25.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Mazungumzo ya Brexit yaanza tena London

LONDON, UINGEREZA

MAZUNGUMZO kuhusu uhusiano wa baadae kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya yameanza tena jana, kukiwa na matumaini finyu ya kupatikana makubaliano ya kibiashara, huku muda pia ukiendelea kuyoyoma wa pande hizo mbili kuepusha kujitenga bila mkataba.

 Mazungumzo ya wiki hii yanafanyika mjini London, baada ya duru ya ana kwa ana wiki iliyopita mjini Brussels, Ubelgiji kumalizika siku moja mapema kutokana na tofauti kubwa katika mkakati wa kila upande. 

Kiongozi wa majadiliano wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier pamoja na mwenzake wa Uingereza, David Frost, walisema tofauti kubwa bado zingalipo, na hiyo inamaanisha pande zote mbili sharti zitafute suluhisho. 

Baada ya kuchukua urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya Jumatano iliyopita, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alisema nchi yake pamoja na umoja huo wenye nchi wanachama 27, zinapaswa kujiandaa kwa hali yoyote endapo makubaliano hayatapatikana.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles