22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mazungumzo ya amani Venezuela yamalizika bila makubaliano

OSLO, Norway

KIONGOZI  wa upinzani   Venezuela, Juan Guaido amesema mazungumzo yanayoandaliwa na Norway baina ya wajumbe wake na wa Rais Nicolas Maduro yataendelea, licha ya awamu ya kwanza kumalizika bila maafikiano yoyote  jana.

 Guaido ameishukuru Norway kwa juhudi zake za kuchangia katika kuutafutia suluhu mzozo wa Venezuela, akiongeza kuwa yuko tayari kuendelea kutoa ushirikiano.

Rais Maduro pia ameunga mkono njia hiyo ya mazungumzo katika hotuba yake iliyotangazwa kupitia  televisheni.

 Katika hotuba hiyo, rais huyo alisema   ana imani katika mjadala, katika kuheshimu katiba na katika amani na demokrasia.

Wawakilishi wa pande hizo mbili katika mzozo wa siasa  Venezuela wamekuwa wakikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza   mjini Oslo.

Hata hivyo  mazungumzo yao yalimalizika  bila makubaliano yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles