24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Malawi yahitaji tani 7,000 za mbaazi

Ramadhan Hassan,Dodoma

Wizara ya Viwanda na Biashara imesema nchi ya Malawi kwa mwaka huu imeonesha uhitaji wa tani 7,000 za mbaazi na taratibu za kihakiki oda hiyo inatekelezwa zinaendelea.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya alibainisha hayo bungeni Leo,Mei 31  wakati akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala(CCM).

Katika swali lake, Mbunge huyo amesema kwa muda mrefu sasa soko la zao la mbaazi nchini limekuwa likisuasua.

“Je nini mpango wa serikali katika kukwamua wakulima wa Mbaazi nchini,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Manyanya amesema mkakati wa muda mfupi ni pamoja na kutafuta masoko mbadala nchi za nje ambapo Mbaazi ghafi zitauzwa.

Amesema kuwa jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda Machi mwaka huu kufuatia ziara ya serikali kutafuta masoko ya mazao ya kilimo ikiwemo Mbaazi katika nchi jirani za Malawi, Burundi, Kongo DRC na Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles