25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Mazingira bora ya kazi na mafanikio ya taasisi- Mafunzo kutoka Exim Bank.  

Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia katika nyanja mbalimbali. Ni Dhahiri kuwa uchumi wa sasa hutegemea sana maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia. Je ipi nafasi ya rasilimali watu na mazingira bora ya kazi katika maendeleo ya taasisi husika?

Kupata majibu ya swali hili, tulifanya mazungumzo na mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa Exim Bank Bwana Fredrick Kanga. Exim Bank ni mshindi wa tuzo za Human Resource Governance and Employee Engagement hapa Tanzania iliyotolewa na Muungano wa Vyama vya waajili Tanzania yaane ATE (Association of Tanznia Employers)

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=jS4kaiSySvU[/embedyt]

Exim Bank inaamini kuwa wafanyakazi bora kwenye mazingira bora ya kazi ndio kiini cha maendeleo ya taasisi husika kwani ndio wanaobuni bidhaa na huduma bora.

“Mimi kama Mkurugenzi wa kitengo cha Rasilimali watu nina husika na kitengo kinachoangalia masuala ya wafanyakazi ambao ndio wanaohusika na kubuni bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kumhudumia mteja vizuri zaidi”. Anasema Fredrick Kanga

Anatoa ufafanuzi zaidi akisema “Kitengo chetu kimepata mafanikio makubwa sana na kuiletea sifa kubwa benki Exim Bank mpaka kiasi cha kutambulika kuwa muajiri bora kwenye yyanja za Utawala wa Rasilimali watu”

Licha ya kutambuliwa kama muajiri bora wa mwaka, Exim Bank bado inaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa inaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wake ili waweze kuwahudumia vyema wateja wao.

“Ni dhamira yetu kuifanya Exim Bank kuwa muajiri bora zaidi nchini kwa kuboresha mazingira ya` kazi na kuongeza ufanisi wa wafanyakazi wetu”. Anamalizia Fredrick Kanga.

Haya ni mafunzo ya muhimu sana kwa taasisi na makampuni binafsi kuwa, pamoja na kuwekeza katika sayansi na teknolojia ni muhimu pia kuwekeza kwenye rasilimali watu, kwani hao ndio wabunifu wenyewe. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,234FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles