31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KASHFA ZATISHIA URAIS WA TRUMP

WASHINGTON, MAREKANI

MWENDELEZO wa kashfa zinazomkabili Rais, Donald Trump, ikiwamo anayodaiwa yeye binafsi alimtaka  Mkurugenzi wa zamani  wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI), James Comey kuachana na uchunguzi dhidi ya mshauri wake wa usalama wa taifa Michael Flynn unatishia urais wake.

Seneta Angus King, ambaye ni mwanasiasa huru japokuwa ameegemea Chama cha upinzani cha Democratic, iwapo taarifa hiyo mpya ni ya kweli uwezekano mkubwa unakuja kwa Trump kung’olewa.

Ikulu  ya  Marekani, White House  ilikana  vikali  baada  ya  dondoo  hizo kuanikwa na kusababisha heka heka za  kupambana  na ripoti zilizoonekana kuwa na madhara kwa utawala  huu mpya.

Taarifa  hizo kutoka kwa James Comey, zilifichuliwa na mtoa habari mmoja aliyeona kitabu cha kumbukumbu cha bosi huyo wa zamani wa FBI.

Taarifa hizo mpya zinakuja wakati utawala wa Trump unaojiingiza matatizoni kila mara ukiwa bado unahangaika  kujisafisha kuhusu taarifa kuwa Trump alitoa  siri nyeti kwa  waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi na balozi wa nchi hiyo  nchini  Marekani.

Wakitetea  hatua  za  Trump, maafisa  walipuuzia  umuhimu na  usiri wa taarifa hizo, ambazo ziliwasilishwa  na  Israel chini ya  makubaliano ya kubadilisha taarifa za kijasusi.

Na Trump  binafsi amesema ana haki zote kama rais  kubadilishana taarifa hizo zinazohusu ugaidi na usalama wa  safari za anga na Urusi.

Pamoja na hayo washirika wa Marekani na baadhi ya wabunge wameeleza wasi wasi wao unaokaribia kuwa tahadhari.

Seneta kutoka Republican, John McCain ametoa matamshi  makali  jana kuwahi  kutolewa  na kambi  ya  chama  hicho anachotoka Trump.

McCain  amesema  hali  hii  sasa imekaribia  kiwango  cha kashfa  kubwa  ya  Watergate.

“Kitu ninachoweza  kusema  ni  kuwa tuliisha  ona  filamu  hii hapo kabla. Nafikiri  inafikia  katika  kiwango  ambapo  ni  sawa  na Watergate na  viwango vya  kashfa  nyingine  ambazo  mimi  na wewe  tumekwisha  shuhudia. “

Comey, ambaye Trump  alimfuta  kazi  wiki iliyopita, aliandika  katika kumbukumbu  baada  ya  mkutano  wa Februari  Ikulu mjini hapa kwamba  rais  mpya  alimuomba  kufunga uchunguzi  dhidi ya Flynn kuhusu mawasiliano   yake na  Urusi.

Uchunguzi kuhusu  Flynn ulikuwa sehemu  ya ule mpana  zaidi kuhusiana  na  Urusi  kuingia  uchaguzi  wa  rais  mwaka  jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles