26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mazembe yaichapa Yanga

TP-Mazembe

Na MWANDISHI WETU-CONGO

TIMU ya soka ya Yanga jana ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja Stade du TP Mazembe, nchini Congo.

Matokeo ya jana yaliiwezesha TP Mazembe iliyokuwa imefuzu hatua ya nusu fainali kufikisha pointi 13 katika Kundi A, huku Yanga ikiondoshwa kwenye michuano hiyo ikiwa imejikusanyia pointi nne.

Hata hivyo, Waarabu wa Algeria, Mo Bejaia walichomoza na ushindi wa bao 1-0 nyumbani na kufikisha pointi nane sawa na Medeama ya Ghana lakini ikayaaga mashindano.

Pamoja na kipigo cha bao 1-0 walichokipata jana, Medeama imetinga hatua ya nusu fainali kwa tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika mchezo wa jana, Mazembe iliandika bao la kuongoza dakika ya 28 kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake, Jonathan Bolingi, aliyeunganisha pasi ya Deo Mukok.

Bao hilo liliongeza kasi ya mashambulizi langoni kwa Yanga hali iliyosababisha mwamuzi, Helder Martins de Carvallo wa Angola kumwonyesha kadi nyekundu, Andrew Vicent ‘Dante’ wa Wanajangwani hao dakika ya 31 baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Mazembe.

Mazembe walikwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0, lakini walianza kipindi cha pili kwa kasi na kuongeza bao la pili dakika ya 55 mfungaji akiwa ni Rainford Kalaba baada ya kupokea pasi safi ya Djo Issama Mpek.

Dakika ya 64, Kalaba aliipatia Mazembe bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Mpek, kabla Yanga kuzinduka dakika ya 75 na kuandika bao la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji wake, Amissi Tambwe.

Bao la Yanga lilitokana na kazi nzuri iliyofanywa na mlinzi wa kushoto, Mwinyi Haji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles