25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Donald Trump ni mgonjwa wa akili

Donald Trump
Donald Trump

Uchunguzi uliofanywa na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford, umebaini kuwa mgombea urais kupitia Chama cha Republican, Donald Trump ni mgonjwa wa akili (hasa mwenye kutumia nguvu).

Utafiti huo ulifanywa hivi karibuni ikiwa ni moja ya namna yakutafuta tofauti ya ushindani kati ya Donald Trump na Hillary Clinton ambaye pia anagombea kiti hicho kupitia chama cha Democratic.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Donald Trump anasemwa kuwa ni mgonjwa wa akili kuliko mpinzani wake Hillary Clinton huku akifananishwa na viongozi wengine ambao wamekuwa na historia ya ukatili na ukarofi kupindukia.

Watafiti hao wamesema kuwa walilinganisha sifa za wagombea hao na kisha kufanainsha matendo yao na viongozi wa kaliba ya ukatili kama Hitler na Saddam Hussein.

Wanaongeza kuwa utafiti wao ulitumia nyaraka zilizopo za maswala ya akili kupata kiwango cha ugonjwa wa akili kwa wagombea hao wawili.

Matokea ya kipimo hicho yanaonesha kuwa Trump alipata asilimia kubwa kuliko Hitler haswa kwa swala la vitisho lakini kuwa chini ya Idi Amin na Henry VIII.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles