30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sarkozy atangaza kuwania tena urais Ufaransa

Nicolas Sarkozy
Nicolas Sarkozy

PARIS, UFARANSA

RAIS wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amethibitisha kuwa atawania tena kiti hicho baada ya kushindwa na Rais wa sasa, Francois Hollande miaka minne iliyopita.

Wakati alipokiri kushindwa kipindi hicho, alisema anastaafu katika ulingo wa siasa, lakini katika kipindi cha miaka miwili alirejea.

Sarkozy ni mmoja kati ya watu wanaowania uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha mrengo wa kati na kulia, wakiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Francois Fillon na Waziri wa Mambo ya Nje, Alain Juppe.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na kesi ya ufisadi na kujaribu kutoa rushwa katika uteuzi wa hakimu wa mahakama kuu, ili atoe taarifa za uchunguzi kuhusu udhamini wa kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles