23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Mawaziri wanane watua Mbeya kuamua hatma ya uhamishaji vijiji Ruaha

Pendo Fundisha, Mbeya

Timu ya mawaziri wanane imekutana Wilayani Mbarali kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la Rais la usitishwaji wa zoezi la kuhamisha vijiji 33 vinavyotakiwa kuondolewa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Wizara hizo ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Wizara ya Utalii na Maliasili, Wizara ya Maji, Wizara ya Muungano na Mazingira, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Mifugo.

Vijiji hivyo viliingizwa kwenye orodha ya kuondolewa baada kubainika kwamba wananchi wake walivamia eneo hilo na kugeuza makazi kinyume cha taratibu na sheria za nchi.

Kutokana na uvamizi huo, Wizara husika ya Utalii na Maliasili iliwasilisha hoja ya vijiji hivyo kuondolewa katika ofisi ya Rais ambaye alisitisha zoezi hilo na kuziagiza Wizara husika kukutana na kufika kwa wananchi kwa ajili ya kuchukua maoni na hatua gani zichukuliwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles