31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakala ACTL wapandishwa kizimbani

PATRICIA KIMELEMETADar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani mawakala wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kuisababishia shirika hilo hasara ya Sh milioni 10.8 pamoja na utakatishaji wa fedha.

Washitakiwa hao ni Farian Ishengoma (34) ambaye ni Mtaalamu wa hali ya hewa na mkazi wa Pasiansi Mwanza, Mawakala wa ndege ni Neema Kisunda (24),  Mkazi wa Pasiansi, Alexander Malongo (29) Mkazi wa Mwanza, Tunu Kiluvya (32) Mkazi wa Mwanza na Job Mkumbwa (30) Nzovwe Mbeya.

Wengine ni wafanyabiashara Adam Kamara (27) Mkazi wa Kiseke, Marlon Masubo (29), Mkazi wa Igoma Mwanza, Mohammed Issah (38) Mkazi wa Yoruba Nigeria, Godfrey Mgomela, Absalom Njusi ja Janetg Lubega ambao walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka katika kesi namba 97/2018 mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Salum Ally, wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai kuwa kati ya Machi 10 na Oktoba 9, mwaka huu katika maeneo ya Dar es Salaam na Mwanza kwa pamoja wakiwa Mawakala wa ATCL waliisababishia shirika hilo hasara ya Sh 10,874,280 kinyume na sheria.

Katika mashitaka ya pili, inadaiwa kati ya Machi 10 na Oktoba 9, mwaka huu katika maeneo ya Dar es Salaam na Mwanza kwa udanganyifu walijipatia fedha hizo kutoka kwa wateja mbalimbali wa ATCL kwa kuwadanganya kuwa watawakatia tiketi.

Pia alidai kati ya tarehe hizo na maeneo hayo, washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuwa walijipatia Sh 10,874,280 mali ya ATCL wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu.

Hakimu Ally alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Wakili Simon alisema kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wamerudishwa rumande hadi Januari 9, 2019 kesi yao itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles