Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Katika msimu huu wa Pasaka, mwimbaji wa Injili kutoka nchini Marekani, Maua Dunia amekata kiu ya mashabiki zake kupitia wimbo, Msalaba.
Akizungumza na mtanzania.co.tz Maua Dunia amewashukuru mashabiki wa muziki huo Afrika Mashariki kwa mapokezi mazuri ya wimbo, Msalaba ambao tayari unachezwa kwenye TV na radio mbalimbali.
“Naushukuru uongozi wangu wa Locha Vision kwa kuendelea kusimama na mimi katika kazi hii ya Mungu, nimeona matokeo makubwa baada ya kuachia wimbo Msalaba chini ya Grevis Records,” amesema Maua Dunia.