29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mashirika yapewa hadi Mwezi Julai kutoa gawio la serikali

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais John Magufuli ameyataka mashirika na Taasisi zinazotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria kuhakikisha hadi kufikia mwei Julai mwaka huu wawe wameshakamilisha zoezi hilo.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi gawio kwa serikali kutoka shirika la masiliano Tanzania TTCL ambapo ameagiza mashirika hayo kuchukuliwa sheria iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.

“Mashirika ambayo hayatoi gawio kila siku ni hasara tu itabidi kutumia sheria na ikishindikana yaondoke maana haiwezekani wao wanaangalia wenzao wakati walipewa mashirika hayo sawa na bure hivyo kabla ya mwezi Julai mashirika yote 253 yanatakiwa yawe yameshafanya hivyo ” amesema.

“Fedha hizi ni ndizo zinazosaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile ujenzi wa barabara, hospitali shule hivyo kwa wale wote wanaotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria wanapaswa kufanya hivyo,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kuendela kuliunga mkono shirika la TTCL kwa kusema kuwa ni la nyumbani lakini pia mapato na faida zitakazopatikana zitatumika kuwasaidia watanzania na kwamba ndio nembo pekee ya kumkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles