23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Marekani yatia hofu vita ya corona

 GENEVA, Uswisi

WINGU la hofu limeendelea kutanda hasa kwa nchi zinazoendelea baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump (pichani), kutishia kusitisha msaada wa taifa lake kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), akilituhumu kutochukua hatua stahiki katika janga la virusi vya corona na kuipendelea China.

Trump alisema hatua hiyo itatekelezwa huku Marekani ikipitia tena jukumu la shirika hilo wakati akidai limeshindwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za kukabliana na Covid-19, kutosema ukweli kuhusu maambukizi hayo.

“Ikiwa WHO ingekuwa imefanya kazi yake ya kutuma wataalamu wa kitabibu nchini China ili kutathmini hali ilivyo, na kuikosoa China kwa kutokuwa wazi, ugonjwa huo ungeweza kudhibitiwa na kutokea kwa idadi ndogo ya vifo,” alisema Trump.

UFADHILI WA LAZIMA NA WA KUJITOLEA

WHO iliundwa mwaka 1948 kama sehemu ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikilenga kuendeleza afya bora, kuhakikisha dunia inakuwa salama na kuhudumia wale walio katika hatari zaidi.

Taasisi hiyo ambayo makao yake makuu ni Geneva Uswisi, ilikuwa na bajeti ya dola bilioni 5.6 kwa kipindi cha miaka miwili (2018-2019), na vyanzo vyake ni viwili tofauti.

Kwanza, kuna pesa ambazo ni lazima zitolewe na nchi washirika 194. Kila nchi inatakiwa kulipa kiwango fulani kulingana na Umoja wa Mataifa kupitia mfumo ambao ni vigumu kuelezeka kwa sababu unazingatia utajiri wa nchi na idadi ya watu. 

 Ni pesa ambayo kwa msingi huwa inasimamia mishahara na utawala wa shirika hilo. 

Mwaka 2018-2019, ufadhili huo ulijumuisha karibia dola milioni 950 za Marekani.

Pili ni ufadhili wa kujitolea unaowezesha nchi na maeneo kuahidi pesa watakazochangia kwa masuala maalumu, kama vile chanjo ya ugonjwa wa polio, afya ya wanawake au ukabilianaji na matumizi ya tumbaku. 

Mwaka 2018-2019, fedha hizo zilikuwa karibia dola bilioni 4.3.

TATIZO

Jack Chow, aliyekuwa balozi wa Marekani katika kukabiliana na Ukimwi na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa WHO, anasema katika miaka ya hivi ya karibu shirika hilo limekuwa likijitegemea kusaidiwa katika kupata raslimali zake ambazo tayari ni sehemu ya bajeti yake. 

“Hili linasababisha matatizo kwasababu ni wafadhili ndio wanaoandaa ajenda zitakazofuatwa na shirika hilo badala ya kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia taaluma,” Chow alisema katika mahojiano na BBC.

Kulingana na taarifa za matumaizi ya fedha za hivi karibuni, Marekani ndio mchangiaji mkubwa wa WHO baada ya kujitolea kufadhili dola za Marekani milioni 893 2018-2019 kwa miaka miwili, ambapo dola milioni 553 za Marekani zimeshatolewa kufikia robo ya nne ya 2019. 

Hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 14.67 ya raslimali zote zilizopokelewa na shirika hilo.

Tofauti na China ambayo ilikuwa imejitolea kutoa dola milioni 86 za Marekani, ambayo tayari imetoa dola milioni 7.9. Ikiwa ni sawa na asilimia 0.21 ya fedha hizo.

Trump anashutumu WHO kwa kushindwa kuzungumza na Serikali ya China kuhusu uchangiaji wao, chimbuko la mlipuko wa sasa wa virusi vya corona. 

Baada ya Marekani, mchangiaji mwingine mkubwa wa WHO ni shirika binafsi la Bill and Melinda Gates Foundation, ambalo liliahidi kutoa dola milioni 530 ambazo tayari limetoa dola milioni 367 million, sawa na asilimia 9.76.

Shirika la Gates lilikosoa amri ya Trump ya kusitisha uchangia wa Marekani kwa WHO.

Mchangiaji mkubwa wa tatu ni GAVI, shirika ambalo linajumuisha mashirika ya umma na serikali ambayo yanapigia upato kuongeza upatikanaji wa chanjo kwa nchi 73 katika maeneo ya kaskazini kote duniani. 

Ufadhili wao ni dola milioni 316 million, asilimia 8.9 ya fedha hizo zilishapokelewa na WHO.

Uingereza ambayo ni mchangiaji mkubwa wa nne, na nchi ya pili ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa huku ikiwa hadi robo ya nne ya 2019 ilikuwa imeshawasilisha dola milioni 294 milioni, sawa na asilimia 7.79 ya bajeti hiyo.

Amerika ya Kusini, nchi zenye kuchangia kwa kiasi kikubwa ni Brazil (dola milioni 35.5 za Marekani), Mexico (dola milioni 13.7 za Marekani) na Argentina (dola milioni 8.5 za Marekani).

ATHARI MAREKANI KUJITOA

Ikiwa Marekani itafanikiwa kutoanza kuchangia, WHO itakuwa na changamoto.

“Uamuzi wa Trump kusitisha ufadhili kwa WHO utakuwa na athari kubwa. Lengo kuu la WHO ni kuzuia kusambaratika kwa mifumo ya afya ambayo ni hafifu kote duniani. Washauri wa WHO wanashirikiana na idara za afya, madaktari wa kijamii na wafanyakazi wa afya kuwasaidia kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

“Hatua ya Trump huenda ikamaanisha kutamatisha miradi mingi ya msingi, kufutwa kazi kwa washauri wengi wa WHO kutoka nchi mbalimbali duniani, pamoja na kwamba watu wengi wa maeneo kama vile Amerika ya Kusini huenda wakawa hatarini sio tu kwasababu ya covid- 19 lakini hata kwa magonjwa mengine mengi kama kifua kikuu na malaria, “ alisema Dk Jack Chow.

MAENEO YANAYOPATA UFADHILI MKUBWA WA WHO 

Kulingana na takwimu zilizochapishwa na WHO hivi karibuni, raslimali iliyotolewa na Marekani kwa miaka miwili 2018-2019 kiwango kikubwa umeelekezwa mashariki ya eneo la Mediterranean, kwa nchi 22 kutoka Morocco hadi Pakistan.

Eneo hilo limepokea karibia dola milioni 201 za Marekani, sawa na asilimia 36 ya pesa zilizotolewa na Washington.

Eneo la pili lenye kupokea kiwango cha juu cha pesa hizo ni Afrika, ambayo inajumuisha nchi 47 kwa bara hilo huku ufadhili kutoka Marekani ukiwa ni dola milioni 151 za Marekani.

Eneo la tatu linalopokea ufadhili wa Marekani ni makao makuu ya WHO, ambayo yanapokea dola milioni 101 za Marekani, kiasi hicho kikitumiwa kwa uendeshaji wa shughuli zake na kampeni kadhaa za masuala ya afya.

Ni asilimia kidogo tu ya ufadhili wa Marekani karibia dola 280,000 sawa na takriban asilimia 0.5, ambazo zimetumika kufadhili shughuli za WHO kwa nchi za Amerika ya Kusini na zile za Caribbean.

Upande wa kampeni za afya, zaidi ya robo ya ufadhili wa Marekani zimetegwa kukabiliana na polio duniani (dola milioni 158 sawa na asilimia 27 ya pesa ilizotoa kwa ujumla).

Pesa nyingine dola milioni 100 zimetumika katika miradi ya kuwezesha watu kupata afya bora na ulaji sahihi, huku dola milioni 44 za Marekani zikitumika katika miradi ya utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika. 

Na dola milioni 33 zinazohitajika kukabiliana na kifua kikuu zikiwa zimeanza kupokelewa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles