23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Maradhi sugu yanayoisumbua Tanzania – 11

woman-in-blue-scrubs-with-hand-on-the-shoulder-of-a-woman-with-stomach-pain

WIKI iliyopita tuliishia katika chanzo cha maumivu wakati wa hedhi.

Leo tunaendelea kuanzia pale tulipoishia…

Hatua hii huchochewa na homoni zenye vitu vinavyojulikana kitaalamu ‘Prostaglandins’ ambavyo huhusishwa na maumivu haya, pia maambukizi katika hatua za juu. Pia vitu vingine ambavyo hujulikana kama ‘Leukotrienes’ hutolewa kwa kiasi kikubwa wakati wa hedhi na kusababisha maumivu wakati wa hedhi.

Dalili za maumivu

Maumivu yanayochoma kwenye tumbo hususan chini ya kitovu.

Maumivu nyuma ya mgongo karibu na kiuno na kwenye mapaja, kichefuchefu na kutapika.

Dalili nyingine ni kutokwa jasho, kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kupata choo chepesi au kukosa kabisa.

Utatambuaje kuwa una maumivu?

Mara nyingi wanawake hujitambua kuwa na maumivu wakati wa hedhi hata bila msaada wa daktari. Kama ni mara ya kwanza inaweza kuwa vigumu kujitambua na hivyo kukulazimu kwenda kumuona daktari, pia kama unahusisha maumivu hayo na tatizo lolote la kiafya. Hapa daktari anaweza kukusaidia kutambua kama maumivu haya yanayotokana na mabadiliko katika mzunguko wa hedhi au ni tatizo la kiafya.

Matibabu

Maumivu wakati wa hedhi hutibiwa na dawa aina ya ‘Anti-prostaglandins’ ambazo hupunguza maumivu katika kuta za mfuko wa uzazi na kufanya hedhi kutoka nyepesi hivyo kukupatia nafuu. Mfano wa dawa hizi ni Ibuprofen au Naproxen.

Wakati mwingine daktari anaweza kutoa vidonge vya uzazi wa mpango ili kuzuia kukua au kukomaa kwa yai la kike na hivyo kupunguza maumivu.

Unawezaje kuyaepuka?

Njia pekee ni kula matunda na mboga za majani, epuka vyakula vya mafuta, pombe, caffeine, chumvi na peremende.

Fanya mazoezi mara kwa mara, epuka au punguza msongo wa mawazo.

Ushauri

Iwapo maumivu yatakuwa makali na pengine kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kuendelea na hedhi kwa siku zaidi ya sita, basi hii ni dalili ya kuwa na tatizo la kiafya. Ninakushauri umwone mtaalamu wa afya kwa uchunguzi na tiba.

200271285-001

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi na maambukizi mengine ya bakteria watokanao na kujamiana. Wakati mwingine uzio (allergy) pia inaweza kusababisha muwasho.

Muwasho maeneo ya  ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (vagina) unaweza kutokana na matumizi ya kemikali, sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria (detergents or soaps), kuosha ndani ya uke na sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema vaginal douching) kitendo hiki husaidia kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda, kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers), sabuni za bafuni (bath products), dawa za usafi kwa akina mama (feminine hygiene products) na njia za uzazi wa mpango.

Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata muwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka, hivyo kusababisha kupata muwasho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles