23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAPATO MADINI YAMEONGOZEKA  KUASHIRIA UJAJI WA MAKAA YA MAWE.

Na Mwandishi Wetu


WAKATI serikali inaendelea na harakati zake za kuboresha sekta ya madini, pato la madini limepanda kwa asilimia nne mwaka 2016/17 kutoka asilimia 3.7 mwaka 2014/15.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema hayo Bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya mapato ya matumizi Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa Fedha 2017/18 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki jana.

Mwijage ambaye aliyesoma hotuba hiyo kutokana na kutenguliwa kwa waziri wake, Profesa Sospeter Muhongo katika sakata la Mchanga wa Dhahabu.

Alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini ni kiasi cha Sh bilioni 131.20 za mrabaha kutoka kwenye migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika, North Mara, Stamigold, TanzaniaOne, Mwadui, Ngaka na Dangote.

Mapato ya kiasi cha Sh bilioni 4.23 kilikusanywa kutokana na mauzo ya dhahabu baada ya kuchenjuliwa, pia kiasi cha Sh billion 4.45 kilikusanywa kutokana na uzalishaji wa madini ya ujenzi na viwanda kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Mwijage alisema kuanzia Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, wizara hiyo ilikusanya mrabaha wa Sh bilioni 5.55 kutoka mauzo ya almasi na Sh bilioni 2.09 kutoka kwenye mauzo ya vito ghafi vilivyokatwa vya Tanzanite, Ganeti, Ruby (yakuti) na Safaya.

Kwa upande mwingine, ajira za moja kwa moja Watanzania  katika sekta madini zimepungua kutoka ajira 7,335 mwaka 2015 hadi kufikia 6,207 mwaka jana  ikiwa nikwa asilimia 15.

Kwa mujibu wa Mwijage, kupungua kwa ajira kwenye sekta hiyo kunatokana migodi kupunguza wafanyakazi husasani wa ajira za muda na mikataba,  kutokana na kushuka kwa bei ya dhahabu na migodi mingine iko njiani kufungwa kama ule wa Buzwagi.

Vilevile ifahamike kuwa kwa zaidinya mwongo mmoja hakuna uwekazaji wowote mkubwa umefanyika  katika sekta ya dhahabu ambako wengi walikuwa wanaajiriwa.

Aidha, idadi ya wataalamu kutoka nje imepungua kutoka 333 mwka 2015 na kufikia 294 mwaka jana sawa na asilimia 12.

Waziri alibainisha kuwa kupitia sekta hiyo serikali iliweza kukusanya kodi ya mapato ya Sh bilioni 79.29 kutoka kampuni kubwa za uchimbaji wa dhahabu nchini.

Waziri a Mwijage alisema kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, jumla ya wakia milioni 1.05 za dhahabu, na wakia 414,128 za fedha na ratili milioni 10.4 za shaba zilizalishwa na kusafirishwa nje ya nchi kutoka migodi ya Stamigold, Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika na North Mara.

Kwa upande wa usalama wa madini alisema hali nchini hairidhishi kwani kwa mwaka wa fedha 2016/17 TMAA ilifanikiwa kukamata madini yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 277.10 katika viwanja vay ndege vya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Songwe yalikuwa yakitoroshwa kwenda nje .

Aidha, Mwijage alibainisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo baadhi ya migodi kutokidhi vigezo ambapo katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Machi mwaka huu, jumla ya ajali 17 zilitokea kwenye migodi na kusababisha vifo vya wachimbaji 30 na haswa katika migodi ya wachimbaji wadogo ambao mara nyingi hawazingatii sheria na mahitaji halisi ya migodi.

Pia serikali ilifanikiwa kuokoa wachimbaji 42  wakiwa hai waliofukiwa katika migodi hiyo.

“Kutokana na wingi wa ajali  katika mwaka 2017/18  wizara itaimarisha ukaguzi wa migodi nchi nzima na kuwa na taarifa ya kila mwezi  za migodi yote inayofanyakazi nchini,”alisema.

Sekta ya madini nchini imekuwa katika hali mbaya baada kupitia ripoti ya tume iliyoundwa na Rais Magufuli ya kuchunguza makinikia kubaini udanganyifu na kuona kiwango kikubwa cha madini ya dhahabu, shaba, fedha, salfa na chuma katika makotena 277 yaliyohifadhiwa bandarini.

Alisema wizara itazingatia mapendekezo yaliyotolewa katika kulinda  madini nchini nakuhakikisha taifa linanufaika kikamili kutokana na rasimali za madini nchini.

Makinikaia yaleta vurumai

Wabunge wengi waliocvhangia hotuba ya bajeti hiyo wameitaka serikali iwe makini katika metendo yake ikizingatia kuwa kamapuni za madini zina gilba na hila za kila aina katika uendeshaji shughuli zake.

Hii ni kutokana na ukweli suala la ‘wizi’ huo limeugawa Bunge Katika amakundi yanayohasimiana kwa kutumiana maneno makali, ya kashfa na yasiyofaa kuelezea suala zima la rasilimali hiyo inayoonekana kuongezeka umaarufu na umuhimu wake kwa uchumi wanchi.

Wabunge waliitaka serikali iruhusu viwanda vya saruji viendelee kuagiza makaa ya mawe kutoka nje ya nchi kwani Kampuni ya Ngaka haina uwezo kuchimba na kupeleka viwandani na vile vile ubora wa makaa hayo kutiliwa mashaka makubwa. Lakini serikali ilisimama kidete na kupuuza madai hayo kwani takwimu zinaonesha inayo uwezo na kwamba hakuna lundo la bidhaa hiyo mgodini ni mwenendo wa uchimaji wake kuzuia mlipuko kama yataachwa wazi kwa muda nrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles