29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Maoni| Jamii ichukue tahadhari kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Na Malima Lubasha, Serengeti

KAMUSI ya Kiswahili Sanifu inabainisha kuwa Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho, kiutu na hata kijamii bila ya kusumbuliwa na ugonjwa wowote.

Maneno hayo ya Kiswahili na misemo mingine mingi tunayosema au kujifunza kwa kusoma maandishi mbalimbali siyo ya kupuuzia lazima tuyazingatiye.

Kila mtu muda wote ili afya yake iwe nzuri anahitaji kufuata taratibu na kanuni bora za afya, zikiwemo kula mlo kamili, chakula chenye virutubisho vyote na kufanya uchunguzi wa afya kwa wataalamu mara kwa mara.

Kuna magonjwa ya aina mbalimbali, yapo ambayo ni yakuambukiza na yasiyoambukiza, moja wapo ya mifano ya magonjwa ya kuambukiza ni UVIKO-19, Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), kipindupindu, homa ya ini na mengineyo mengi.

Baadhi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, kisukari, saratani, seli mundu, mishipa ya damu.

Licha ya kuwepo magonjwa hayo, Serikali imeendelea kutoa elimu kwa watu wake namna bora ya kukabi liana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali  ya afya.

Katika kukabiliana na hali hii, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hivi karibuni alitoa tamko na kusema magonjwa yamekuwa yakiongezeka na kusababisha vifo kwa Watanzania kutokana na kuiga mifumo ya maishaya watu wan chi za Magharibi.

 Alisema miongoni  mwa magonjwa yasiyoambukiza ni saratani na homa ya ini ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa haraka kulingana na utafiti uliofanywa .

Waziri Ummy alisema ni vema tukaipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhi Hassan, kwa kutaka kuanzisha kampeni maalum ya kutoa chanjo kwa wasichana chini ya miaka 14.

Alisisitiza kuwa jamii ijue homa ya ini,kwa sasa ni hatari kuliko UKIMWI ambao maambukizo yake ni asilimia nne, lakini homa ya ini ni asilimia tano, inaambukizwa kwa kujamiana na hata kwa jasho kama vile kupeana mikono na mwenye ugonjwa huo.

Kila mtu atambue umuhimu wa afya yake, kila wakati endapo unahisi kuumwa na kitu chochote, unapaswa kwenda hospitali kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya yako, tusiwe tunadharau magonjwa bila kujali lina ukubwa wa athari gani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles