23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Manispaa yakanusha kutoa chanjo ya corona

Na Walter Mguluchuma, Sumbawanga

Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imekanusha uvumi ulioenea kuwa leo inaanza kutoa vidonge ambavyo ni kinga ya ungonjwa wa Covid-19 kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari katika Manispaa hiyo.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Manispaa hiyo, Veronica Maula alisema kuwa vidonge vitakavyo tolewa shuleni kwa wanafunzi ni kingatiba kwa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo ni pamoja na minyoo ya tumbo na kichocho.

Amesema kuwa dawa hizo zimekuwa zikitolewa kila mwaka na mpango huo ulianza mwaka 1998, na kila mwaka wanafunzi wamekuwa wakipewa hivyo basi ni vizuri wazazi wakazingatia kuwapa chakula watoto wao, lakini pia kuwe kuna mpango wa wanafunzi kupata chakula shuleni kabla ya kumeza dawa hizo.

Mratibu huyo wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Manispaa ya Sumbawanga aliwataka wazazi kutowazuia watoto wao kupata vidonge hivyo vya kinga tiba kwani ni muhimu Sana vimekuwa vikiwakinga dhidi ya magonjwa hayo na Kama wanaugua magonjwa hayo dawa hizo zimekuwa zikiwatibu.

Alitoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo kuacha kusikiliza uvumi uliopo mitaani badala yake wasikilize maelekezo kutokwa kwa wataalamu kwani masuala ya afya ni mambo ya kitaalamu si yakuanzia vijiweni kwani kumekuwa na upotoshwaji mkubwa katika baadhi ya mambo.

Zoezi la utoaji dawa kwaajili ya kukinga na kuzuia magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa linafanyika leo ambapo litawahusu wanafunzi wa kuanzia miaka mitano na kuendelea ambapo wanafunzi wote watapatiwa dawa hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles