24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo akutana na Mzee Msekwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amekutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho Mzee Pius Msekwa katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba na kumuahidi kukitumikia, kukisimamia na kuimarisha zaidi CCM.

Chongolo amemhakikishia Mzee Msekwa kuwa Chama kipo salama chini ya Sekreterieti anayoiongoza na kwamba Katiba, Kanuni, taratibu na miongozo ya Chama iliyowekwa na Waasisi wa CCM itaendelea kuheshimiwa, kulindwa na kufuatwa, na kwamba Jahazi la CCM chini ya uongozi wake halitakwenda mrama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo(Kulia) akizungumza na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Mzee Pius Msekwa leo Mei 24, 2021 Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Chonholo ameeleza kuwa mafunzo ya uongozi, utawala na siasa aliyoyapata wakati wote akiwa mtumishi kwenye Chama na Serikalini yamemkomaza na kumuandaa vyema kwa nafasi aliyoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan.

Chongolo amemueleza Mzee Msekwa kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Wazee wastaafu aliobahatika kufanya kazi chini yao, amejifunza Ujasiri, kujiamini na kupata upeo na maarifa ya kutosha.

“Nakushukuru sana Mzee Msekwa, wewe na viongozi wenzako wastaafu kwa jinsi mlivyonilea. Nimechota maarifa na kujifunza mengi kutoka kwenu na kuniandaa.

“Nichukue nafasi hii kukuhakikishia kwa fikra zile zile, nidhamu ile ile na misimamo inayozingatia  mabadiliko ya nyakati CCM kitaendelea kubaki chama bora Barani Afrika,” amesema Chongolo.

Chongolo amesema licha ya kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha ataendelea kujifunza zaidi. Amesema kila atakapokwama hatosita kukimbilia kwao kwa ushauri na elimu ya uongozi.

Kwa upande wake Mzee Msekwa amesema CCM hakijawahi kumkabidhi mwanachama wake yeyote dhamana ya kuongoza hata ofisi ya tawi ikiwa mtu au mwanachama huyo hatoshi na hana vigezo.

Hivyo akamuhakikishia, Chongolo kuwa Mwenyekiti wa CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wamejiridhisha kuwa anatosha, akamshauri aonyeshe utiifu, nidhamu na kukisimamia chama kwa uamunifu na kupokea na kuzingatia maelekezo atakayopewa na Mwenyekiti na Vikao vya Chama.

“Una wajibu  wa kuhakikisha Sekreterieti yako muda wote mnakuwa na msimamo  wa pamoja. Una kazi ya kutekeleza maagizo aidha ya H/kuu ya Taifa au ya Kamati Kuu ya CCM na kutekeleza” amesema Mzee Msekwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles