30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

MANISPAA ILALA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO

 

 

CHRISTINA GAULUHANGA

NA SAID ABDALLAH (OUT)

BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Ilala limesema licha ya kupokwa vyanzo vya mapato, limefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo ya mapato walilojiwekea katika mwaka 2016/17.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam, katika kikao cha Baraza la Madiwani wa manispaa hiyo na Naibu Meya, Omary Kumbilamoto (CUF).

Alisema walipanga kukusanya Sh bilioni 13.5 kwa mwaka ambako hadi sasa katika robo nne ya mwaka wamekusanya tayari Sh bilioni zaidi ya 13.5.

“Mbali ya kupitia changamoto za watumishi hewa, vyeti feki, kupokonywa ukusanyaji kodi za majengo, tumeathirika katika utendaji na uchumi kuyumba, lakini hata hivyo tumejitahidi kuvuka lengo,” alisema Kumbilamoto.

Alisema hali ngumu ya uchumi imepunguza kasi ya ongezeko la biashara mpya na kusababisha biashara nyingi kufungwa na kuhama.

Kumbilamoto alisema ucheleweshaji wa ruzuku kutoka serikalini nayo ni sababu kubwa ya manispaa kushindwa kutekeleza baadhi ya miradi kwa wakati.

Alisema hata hivyo, halmashauri na madiwani wanatakiwa kuibua vyanzo vipya vya mapato kuifanya manispaa hiyo kuwa endelevu.

Meya wa Manispaa ya Ilala (Chadema), Charles Kuyeko, alisema bado kuna upungufu wa madawati katika shule za msingi za manispaa hiyo, kwa sababu ya ongezeko la wanafunzi wanaohamia.

“Ongezeko la ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa linasababisha pia uhaba wa madawati,” alisema Kuyeko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles