30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

MAN UNITED YAPIGWA FAINI MILIONI 53/-

MANCHESTER, ENGLAND

CHAMA cha Soka nchini England (FA), kimeipiga faini klabu ya Manchester United kwa wachezaji wake kuonesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea, Jumatatu wiki hii.

Katika mchezo huo kiungo wa klabu ya Manchester United, Ander Herrera, alioneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kumchezea vibaya Eden Hazard, lakini kitendo hicho kiliwafanya wachezaji wa klabu hiyo kumzonga mwamuzi, Michael Oliver kwa madai haikuwa kadi sahihi.

Kutokana na hali hiyo, Chama cha soka nchini humo kiliifungulia mashtaka klabu hiyo tangu Jumanne, lakini juzi walitoa maamuzi ya kuwapiga faini ya pauni 20,000, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 53 za Tanzania.

Katika mchezo huo Manchester United walikubali kuyaaga mashindano baada ya kuchezea kichapo cha bao 1-0, likiwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji, N'Golo Kante.

Chama hicho cha soka kimeweka wazi kwamba, uongozi wa klabu ya Manchester United umekubali kuwa ulishindwa kuzuia wachezaji wake kufanya fujo katika dakika ya 35.

“Manchester United wamepigwa faini ya pauni 20,000 baada ya kukubali kuwa ilishindwa kuwazuia wachezaji wake, hivyo wapo tayari kulipa faini hiyo. Wachezaji hao walivunja sheria kifungu cha E20 (a),” waliandika FA.

Katika mchezo huo wengi walidhani kuwa Mourinho atakuwa wa kwanza kumtupia lawama mwamuzi kutokana na tabia zake za kuwashambulia waamuzi, lakini alidai wachezaji wake walikosa bahati.

“Msimu huu mwamuzi Michael Oliver, ameonesha kiwango kizuri, lakini niweke wazi kuwa wachezaji wangu walikosa bahati katika mchezo huo dhidi ya Chelsea.

“Katika michezo minne iliyopita ameweza kutoa penalti tatu na kadi nyekundu moja, lakini naweza kusema ilikuwa kadi ya mapema sana, ila siwezi kubadili kilichotokea,” alisema Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles