27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SERA YA UHAMIAJI KUBADILISHWA AFRIKA KUSINI


HH, MAREKANI

SERIKALI nchini Afrika Kusini, imetangaza kufanya mabadiliko katika sera zake za uhamiaji ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na machafuko ya mara kwa mara yanayosababisha wageni kushambuliwa na wenyeji.

Kati ya sera hizo ni pamoja na kutengeneza vituo vya kushughulikia wanaoomba hifadhi ya ukimbizi kupitia mipaka ya nchi hiyo.

Hii inaashiria mwisho wa uhakika wa kupata uraia baada ya kuwa mkazi wa muda mrefu nchini humo. Pia kuanzishwa kwa utaratibu wa pointi unaokusudia kuwavutia wahamiaji wenye ujuzi na kuondoa baadhi ya masharti ya viza kwa raia wa Kiafrika.

Pendekezo la mabadiliko hayo limekuja wakati nchi ikiwa imeghubikwa na chuki na vitendo vya uvunjifu wa sheria dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika, hali kukiwa na maoni kwamba hilo si jambo linalopendeza na wala haiwezekani kuzuia uhamiaji wa kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Malusi Gigaba, amesema pendekezo hilo ambalo litapelekwa mbele ya bunge wiki ijayo, linakusudia kuweka uwiano unaoridhisha kati ya kuwakaribisha wahamiaji wengi kutoka nchi za Afrika na kuhakikisha usalama wa taifa.

Sera hiyo mpya imekuja wakati kumekuwa na wimbi la uvunjifu wa amani katika wiki za karibuni dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika ambao waandamanaji wanaochukua sheria mikononi mwao wanawatuhumu wahamiaji kwamba wamechukua kazi zao na rasilimali chache kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini.

Mwaka jana, Idara ya Mambo ya Nje ilisema watu milioni 16 waliwasili Afrika Kusini. Wengi kati yao wametoka nchi za jirani zikiwemo Lesotho, Zimbabwe, Msumbiji, Swaziland na Botswana.

Aidha, Serikali nchini humo ilisajili kuwasili kwa zaidi ya Wamarekani 400,000 na zaidi ya raia wa Uingereza 560,000. Mwaka huo huo, maofisa wa uhamiaji waliwasafirisha zaidi ya watu 23,000, wengi wao kutoka Msumbiji, Zimbabwe, Lesotho, Swaziland na Malawi.

Mkurugenzi wa Tume ya Uhuru wa Watu Kutembea (nchi moja hadi nyingine) kwa jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, Tony Elumelu, amesema sera iliyopendekezwa na Afrika Kusini itafanya kazi vizuri kutokana na hali ya wahamiaji wa kimataifa wanaopita nchini.

Hata hivyo, wanaharakati wa haki za binadamu wameeleza wasiwasi wao juu ya mapendekezo mapya ya Serikali. Jacob van Garderen, mkurugenzi wa taifa wa mawakili wa haki za binadamu, amesema pendekezo hilo juu ya wanaoomba hifadhi ya ukimbizi wana wasiwasi nalo.

Waziri Gigaba atawasilisha mapendekezo hayo kwenye Baraza la Mawaziri la Afrika Kusini wiki ijayo. Amesema ana mategemeo makubwa kwamba itapitishwa na mabadiliko hayo yataanza kutumika mwaka 2018.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles