23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Man United watalipa kisasi kwa Barcelona leo?

BARCELONA, HISPANIA

KIVUMBI cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kinatarajia kuendelea leo hatua ya robo fainali baada ya michezo mingine kupigwa jana, leo Barcelona watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Man United ambao waliwachapa kwenye fainali mbili.

Huu ni moja kati ya michezo ambayo itakuwa ya kisasi kutokana na historia ya nyuma walivyokutana, Barcelona wamekuwa wababe wa wapinzani hao hasa kwenye hatua hizo za juu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barcelona waliwachapa Man United mwaka 2009 katika fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0, yaliwekwa wavuni na Samuel Eto’o na Lionel Messi na kutwaa ubingwa huo.

Msimu uliofuata Barcelona waliendeleza ubabe wao kwa kutwaa ubingwa huo kutokana na ushindi wa mabao 3-1, huku mabao hayo yakifungwa na Messi, Pedro Rodriguez pamoja na David Villa, wakati huo bao la Man United likifungwa na Wayne Rooney.

Wachezaji waliobaki ndani ya Barcelona ambao waliongoza katika safu ya ushambuliaji na kupata mabao hayo, amebakia Messi ambaye alifunga katika fainali zote mbili walizokutana na leo wanakwenda kukutana kwenye robo fainali.

Kumbukumbu zinaonesha timu hizo zimekutana mara 11 katika historia yao, huku Man United ikishinda mara tatu, lakini Barcelona wamekuwa wababe zaidi.

Messi amefunga jumla ya mabao 22 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akizifunga timu za England na kuwa mchezaji wa kwanza kuwa na mabao mengi ya michuano hiyo kwa kuzifunga timu hizo za England.

Mchezo huo unaweza kumpa heshima kubwa kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, endapo United itafanya vizuri. Kocha huyo alipewa jukumu hilo tangu Desemba mwaka jana akichukua nafasi ya Jose Mourinho, lakini kitendo hicho cha kupangiwa Barcelona ambao wamekuwa na uzoefu mkubwa wa michuano hiyo, kinaonekana kama ndio mwisho wa Man United japokuwa waliishangaza dunia kwa kuwaondoa wababe wa soka nchini Ufaransa, PSG.

Mchezo mwingine ambao utapigwa leo ni pamoja na Ajax ambao watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha Juventus. Japokuwa Juventus walionesha ubora wa hali ya juu katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid baada ya kuwafunga mabao 3-0, huku mchezo wa kwanza Juventus wakifungwa mabao 2-0, bado Ajax wanaogopwa kutokana na aina ya uchezaji wao.

Ajax wamefika hapo baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Real Madrid kwa jumla ya mabao 5-2, huku mchezo wa kwanza Ajax wakiwa nyumbani na kufungwa mabao 2-1, lakini marudiano kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu waliweza kupindua meza kibabe na kushinda mabao 4-1.

Kutokana na hali hiyo, Ajax bado wanaonekana kuwa tishio kwa Juventus na wakiwa na lengo la kutaka kulipiza kisasi cha mwaka 1996 kwenye fainali za michuano hiyo, ambapo dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 1-1, lakini Ajax wakaja kukubali kichapo cha mabao 4-2 ya mikwaju ya penalti.

Habari njema kwa Juventus ni uwepo wa mshambuliaji wao, Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja, lakini hata kama atacheza mchezo huo, basi anaweza asiwe fiti kwa kiasi kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles