30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Diego Costa kufungiwa michezo nane

MADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Atletico Madrid, Diego Costa, anaweza asionekana tena kwenye michuano ya Ligi Kuu Hispania msimu huu kutokana na kuwa hatarini kufungiwa michezo nane kwa kumtukana mwamuzi.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Hispania, mchezaji huyo anafanyiwa uchunguzi wa maneno yake ambayo aliyatoa kwa mwamuzi, Jesus Gil Manzano, katika mchezo wao dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou, huku Atletico wakikubali kichapo cha mabao 2-0.

Mchezaji huyo alioneshwa kadi nyekundu moja kwa moja kwa utovu wa nidhamu, pia alionekana akitoa maneno machafu kwa mwamuzi huyo, hivyo kutokana na kadi hiyo, anatakiwa kusimamishwa michezo miwili, lakini kutokana na maneno yake ya matusi, anaweza kuongezewa adhabu na kufikia michezo nane.

Endapo atakutana na adhabu hiyo, basi mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu hadi mwisho wa msimu huu.

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Hispania, inatarajia kukutana leo kwa ajili ya kujadili tukio hilo na kutoa maamuzi.

Katika ripoti ya mwamuzi huyo, aliweka wazi kuwa, Costa alimtukana zaidi ya mara moja, hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo, mwamuzi aliongeza kuwa, kuna wakati alimshika mkono mwamuzi huyo ili asitoe kadi ya njano kwa mchezaji mwenzake jezi namba 24 (Jose Gimenez) pamoja na jezi namba 2 (Diego Godin).

Hadi sasa imesalia michezo saba kumalizika kwa michuano ya Ligi Kuu Hispania, hivyo mchezaji huyo akichukuliwa hatua, anaweza kuja kuonekana tena wakati wa kiangazi, lakini inategemea kama timu hiyo itaendelea kuwa na mchezaji huyo au itaamua kumuuza.

Costa amecheza jumla ya michezo 21 ya Atletico Madrid msimu huu kati ya 41 ya michuano mbalimbali, amefanikiwa kupachika mabao matano, alioneshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Juventus hatua ya 16 bora katika mchezo wa awali na kuwafanya wawe katika wakati mgumu kwenye mchezo wa marudiano na wiki iliyopita akaoneshwa kadi nyingine nyekundu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles