26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Man City kuendelea kukaa kileleni leo?

1344210-28878056-1600-900MANCHESTER, ENGLAND

MICHUANO ya Ligi Kuu nchini England inatarajia kuendelea leo katika viwanja mbalimbali, huku Stoke City wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha vinara wa michuano hiyo, Manchester City.

Huu ni mchezo ambao utatazamwa sana kutokana na nafasi hiyo ambayo inashikiliwa na Manchester City ikiwa ipo sawa na Leicester City, wote wakiwa na alama 29 katika msimamo wa Ligi, wakitofautiana mabao.

Mchezo huu Man City watautolea macho ili waweze kuondoka na alama tatu na kuwaombea dua mbaya wapinzani wao, Leicester City wapoteza mchezo wao wa ugenini dhidi ya Swansea City.

Endapo Manchester City wataupoteza mchezo huu basi watawapa nafasi wapinzani wao ambao wanawania nafasi hiyo kama watafanikiwa kushinda michezo yao ambao ni Manchester United wenye alama 28, Arsenal alama 27 na Leicester City wakiwa na alama 29, sawa na Man City.

Hata hivyo, kwa upande wa Leicester wao pia watahakikisha wanashinda katika mchezo wao dhidi ya Swansea City ili kuzidi kujiwekea rekodi ya kukaa kileleni katika michuano hiyo na kuzishusha timu kongwe.

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Arsenal dhidi ya Sunderland, Man Utd dhidi ya West Ham, wakati Southampton ikipambana na Aston Villa, Watford itavaana na Norwich, West Brom itakutana na Tottenham, wakati huo Chelsea ikiwa nyumbani dhidi ya Bournemouth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles