KLABU ya Manchester United imepata pigo baada ya beki wake Marcos Rojo kufyatuka bega akiwa mazoezini na klabu hiyo.
Ajalia hiyo ya kufanyatuka bega ilitokea wakati wa mazoezi juzi ambapo aliumia bega lile lile aliloumia msimu uliopita katika mchezo dhidi ya Manichester City na kukaa nje ya Uwanja kwa wiki nne.
Hata hivyo klabu hiyo bado haijazungumzia suala la beki huyu ila kocha wa timu hiyo Louis van Gaal anatarajia kutoa maelezo ya kuumia huko kwa beki wake.
Beki huyo kisiki alisajiliwa mwaka 2014 akitokea timu ya Sporting Lisbon ya Ureno kwa dau la Pauni Milion 16, anaungana na beki mwingine wa kushoto Luke Shaw anayeuguza jeraha la kuvunjika mguu mara mbili.
Manchester United inatarajiwa kushuka dimbani leo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham kwenye Uwanja wa Old Trafford, huku ikipigania nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi.