29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

MAMILIONI YA WACATALONIA WAANDAMANA

BARCELONA, HISPANIA


MAMILIONI ya wakazi wa Catalonia wameandamana jana katika mitaa ya eneo hilo kulalamikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa wakati wa kura ya maoni wiki iliyopita.

Hispania imeitaja kura hiyo ya maoni kuwa ni kinyume cha sheria japo zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga kura.

Lakini mamia ya watu walijeruhiwa wakati polisi wa Hispania walipokuwa wakijaribu kuzuia zoezi hilo kuendelea.

Baadhi ya maofisa walioamrishwa kuwazuia watu wasipige kura, walionekana wakifyatua risasi za mipira, wakivamia vituo vya kupigia kura na kuwavuta nywele wanawake.

Maandamano hayo ya jana yalisababisha kufungwa kwa barabara kubwa, baa, maduka, migahawa, huku pia milango ya ofisi za serikali ikiwa imewekewa vizuizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles