28.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAHAHA KUSAKA CHANZO CHA MAUAJI LAS VEGAS

LAS VEGAS, MAREKANI


POLISI wa Marekani, wanahaha kutafuta chanzo cha shambulio la risasi lililosababisha vifo vya watu 59 na kujeruhi wengine 527 kwenye tamasha lililokuwa likifanyika huko Las Vegas, nchini humo.

Mtu mwenye silaha aliyejulikana kwa jina la Stephen Paddock (64), alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya Hoteli ya Mandalay Bay, akiwalenga wapenzi wa muziki waliokuwa wakijimwaya kwenye tamasha hilo la muziki wa ‘country’ Jumapili usiku.

Polisi walipata bunduki 23 kwenye chumba cha muuaji huyo kwenye hoteli hiyo na nyingine 19 nyumbani kwake huko Nevada.

Lakini hadi sasa hakuna sababu hasa iliyobainika kuchangia shambuliao hilo kwani wachunguzi hawajapata uhusiano wowote na ugaidi japo kundi la Islamic State limedai kuhusika.

Baadhi ya wachunguzi wamedai mtu huyo kuwa na matatizo ya kisaikolojia, lakini hilo bado halijathibitishwa.

Paddock aliishi katika jamii ya watu wazima kwenye mji mdogo wa Mesquite, Kaskazini Mashariki mwa Las Vegas na kwamba aliripotiwa kuishi na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Marilou Danley ambaye kwa sasa yuko nchini Japan na polisi wanasema inawezekana mwanamke huyo hakuhusika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles