31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

TUME YA UCHAGUZI KENYA KUWAKUTANISHA ODINGA, UHURU

NAIROBI, KENYA


TUME ya Uchaguzi Kenya (IEBC), imeitisha mkutano wa wagombea urais nchini humo ambao utawahusisha kiongozi wa upinzani, Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Mkutano huo umepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya, jijini Nairobi.

IEBC imeitisha mkutano huo na wagombea hao wakuu wa urais kabla ya uchaguzi wa Oktoba 26, mwaka huu, kujadiliana kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo.

Tume hiyo imetoa mwaliko huo, ikiwa ni siku moja baada kufanya mazungumzo na wajumbe 12 kutoka nchi za kigeni, wakiongozwa na Balozi wa Marekania nchini Kenya, Robert Godec na naibu balozi wa Uingerzea nchi humo, Susie Kitchens, ambao wamewataka wanasiasa kuheshimu uhuru wa IEBC.

Baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati ya wawakilishi wa Chama cha Jubilee, Chama cha National Super Alliance (NASA) na IEBC Alhamisi ya wiki iliyopita, Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati, alisema alitaka kukutana ana kwa ana na wagombea wakuu akiwalaumu wawakilishi wao kwa misimamo mikali.

Wakati huo huo, Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kwasababu za kiusalama kwa mujibu wa viongozi wa chuo hicho.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi ndani ya chuo hicho.

“Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka mara moja kabla ya saa tatu asubuhi (jana),” ilisema taarifa ya chuo hicho.

Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho, Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino.

Owino, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Embakasi Mashariki, jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles