23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Malkia akaunti ya CRDB yawezesha wanawake kumiliki viwanja Butiama

Na Shomari Binda, Butiama

WANAWAKE mkoani Mara wamesema utunzaji wa akiba kupitia akaunti ya malkia ya benki ya CRDB imewawezesha kumiliki viwanja.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani Butiama, mkoani Mara wanawake hao wamesema kujiwekea akiba ni mwanzo wa mafanikio.

Wamesema kabla ya kufungua akaunti hiyo walipata elimu kutoka benki ya CRDB tawi la Musoma juu ya umuhimu wa Malkia akaunti na kuamua kufungua.

Mmoja wa wanawake hao, Mariamu Juma, amesema ameweza kumiliki kiwanja na kupata hati ya kumiliki kutokana na kuweka akiba kupitia Malkia akaunti.

Mariam amesema mwanamke mpambanaji anaweza kumiliki kiwanja na mali iwapo atakuwa na malengo ya kuweza kufanya jambo.

Amesema benki ya CRDB kupitia akaunti ya Malkia inayo malengi mazuri kwa mwanamke katika kumuwezesha kupitia akiba anayoiweka kwa ajili ya baadae.

“Naishukuru benki ya CRDB kwanza kwa elimu ya ujasiriamali niliyoipata Musoma na baadae kufungua akaunti ya Malkia.

“Akiba niliyoiweka kupitia akaunti hii imeniwezesha kumiliki kiwanja na kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake nimeweza kukabidhiwa hati ya kumiliku,” amesema Mariam.

Kwa upande wao watumishi kutoka benki ya CRDB walioshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Butiama wamesema bado fursa ipo kwa wanawake kuweza kujiunga na akaunti ya Malkia kwa kuwa inamanufaa makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles