23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Watu watatu wafariki dunia baada ya lori la mafuta kugongana na gari dogo Songwe

Na Denis Sinkonde, Songwe

Watu watatu wamefariki Dunia na miili yao kuteketea kwa moto katika ajali, baada ya Lori la mafuta lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Zambia kuligonga gari dogo kisha kulipuka moto akiwepo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi, Mchungaji Willy Mwasile.

Tukio hilo lilitokea Machi 7, 2022 saa 9:45 mchana katika mtelemko wa Old Vwawa, jirani na shule ya sekondari ya kutwa ya Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Akizungumzia tukio hilo mara baada ya kushiriki zoezi la uokoaji na kutoa mabaki ya miili ya marehemu kwenye magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba, amesema chanzo cha ajali hiyo ni lori kumshinda dereva na kuanza kuyumba na kwenda kuligonga gari dogo lililokuwa limembeba Mwenyekiti wa Kanisa la Moraviani Tanzania, Jimbo Kuu la Mbeya, Mchungaji, Willy Mwasile na familia yake ya watu watatu.

“Katika gari dogo alikuwepo Mchungaji Mwasile ambaye amejeruhiwa, watoto wadogo wawili ambapo mmoja amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto na mwingine kujeruhiwa, pamaoja na dereva wao.

“Katika gari dogo kulikuwa na Baba mchungaji Mwasile na familia yake walikuwa wakitokea Tunduma kwenda Mbeya tumetoa mabaki ya mwili wa mtoto mdogo ukiwa umeteketea vibaya kwa moto, kadhalika na kwenye lori nako tumetoa mwili ukiwa umeteketea kwa moto,” amesema Mgumba na kuongeza kuwa;

“Hata hivyo, tumeshindwa kuthibitisha kama mabaki ya mwili yaliyotolewa kwenye lori ni ya dereva au mtu mwingine aliyekuwa kwenye gari hilo, licha ya kupata nyaraka za dereva (Leseni na hati ya kusafiria) zikiwa zimeokotwa eneo la tukio zikiwa salama hazijaungua” ameongeza Mgumba.

Kaimu Kamanda Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani, amesema ajali hiyo ilihusisha magari mawili ambayo ni lori la mafuta lenye namba za usajili T 908 CWA na trela lake namba T 231 CWA mali ya Kampuni ya ASAS ya Iringa.

Lori hilo lilimshinda dereva na kwenda kuligonga gari dogo aina ya Pajero Mitsubishi lenye namba T 301 DTE mali ya Kanisa la Moravian jimbo kuu la Mbeya.

Kaimu Kamanda Ngonyani amesema majina ya marehemu wote hayakupatika, licha ya kwamba walipata nyaraka muhimu za dereva lakini hawezi kuthibitishwa kuwa ndiye aliyeteketea kwa moto.

Aliwataja majeruhi kuwa ni, pamoja na Mchungaji Mwasile, Dereva wa mchungaji Mwasile, Allen Mbabala, Augustino Very Sichalwe (15) pamoja na marehemu anayekadiliwa kuwa na miaka (9).

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Vwawa, Willson Kasenga, alisema walipokea majeruhi watatu ambao waliwapatia matibabu ya awali, lakini kutokana na hali zao wamepewa rufaa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa kati ya majeruhi waliopewa rufaa akiwepo mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi willy Mwasile.

1. PICHA YA KWANZA MKUU WA MKOA WA SONGWE AKIWA ENEO LA TUKIO
2.PICHA YA PILI GARI LIKIWAKA MOTO.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles