24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Malezi hafifu ya wazazi chanzo cha msongo

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

USHIRIKI hafifu wa wazazi kwenye malezi umetajwa kuwa changamoto na chanzo cha msongo wa mawazo kwa watoto na vijana nchini.

Aidha,ugumu wa maisha nao umeelezwa kama kichocheo za wazazi wengi kuwa wakali na kusahau misingi ya malezi bora kwa watoto.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Oktoba 14 na Balozi wa Vijana kutoka Tanzania, Faudhia Kitenge, kwenye Jukwaa la sita la REPSSI linalofanyika mjini Maputo, Msumbiji likihusisha nchini 13 ambapo Tanzania inashiriki kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya Uviko-19.

Faudhia ambaye ni balozi kupitia REPSSI Tanzania amesema kuwa nyakati kwa sasa zimebadilika hivyo wazazi wanapaswa kutimiza jukumu lao la malezi na kuepusha watoto kulelewa na mitandao ya kijamii.

“Tumewasilisha changamoto nyingi kama watoto na vijana kwa nchi yetu ya Tanzania,miongoni mwa hizo ni pamoja na wazazi wengi kusahau majukumu yao kwa kujikita kwenye kusaka fedha na hivyo kusababisha watoto kulelewa na mitandao ya kijamii kutokana na kukosa taarifa sahihi,” amesema Faudhia.

Faudhia ameongeza kuwa changamoto nyingine ni ukesefu wa taarifa sahihi kwa watoto kuhusu janga la uviko-19 hatua iliyochochea zaidi ukatili.

“Kutokana na mambo mengi ambayo yanayotokea kwenye jamii zetu za kiafrika unakuta changamoto ya msongo wa mawazo, magonjwa ya afya ya akili ni tatizo kubwa kwa vijana ikiwamo malezi.

“Hivyo tumezungumzia mambo mbalimbali ikiwamo changamoto ya uviko-19, ukatili wa kijinsia, elimu na ulinzi,hivyo kulikuwa na upotoshaji mkubwa kwa vijana hususan wa vijijini ambao walikuwa hawapati taarifa ikilinganishwa na wenzao wa mijini.

“Kama hiyo haitoshi, wakati watoto wanarudi nyumbani kutoka shule sababu ya Uviko-19, hii iliibua changamoto nyingine kwenye familia ikiwamo ubakaji na ukatili pasi kuwa na msaada wa kisaikolojia,hivyo vijana walikosa taarifa sahihi kwa wakati sahihi,” amesema Faudhia.

Upande wake, Afisa Ustawi Mkuu, kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Darius Kalijongo amesema wazi wengi kwa sasa wamekuwa hawazingatii misingi ya malezi bora jambo ambalo limezidisha migogoro na msongo wa mawazo kwa vijana.

“Hali ya watoto Tanzania siyo nzuri kwani matendo ya ukatili yanazidi kuongezeka kila kukicha, lakini kama hiyo haitoshi baadhi ya wazazi hata ile misingi ya ukuaji wa watoto hawaifahamu.

“Wengi wa wazazi wanakiuka misingi bora ya malezi kuanzia mwanzo kabisa mtoto anapokuwa tumboni hatua ambayo imekuwa ikileta madhara makubwa baadaye, watoto hawapewi haki ya kufanya mambo yanyowapasa kulingana na ukuaji wao,” amesema Kalijongo.

Amesema upande wao kama serikali wanaendelea kuandaa mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wawazazi wanatimiza wajibu wao wa maelezi kwa ustawi thabiti wa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles