30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yapania kufikia wateja milioni 10 ifikapo 2023

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu ya Viettel au maarufu Halotel, inayojikita kupeleka mawasiliano vijijini , leo imetimiza miaka sita ya kutoa huduma hapa nchini huku ikidhamiria kufikisha idadi ya wateja milioni 10 kufika mwaka 2023.

Akizungumza na Dar es salaam leo Ijumaa Oktoba 15, Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Halotel, Abdallah Salum, amesema kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka sita.

Amesema kuwa katika kipindi hicho Kampuni imekuwa ikisajili wateja zaidi ya milioni moja kwa mwaka na kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2021, Kampuni imeweza kusajili wateja milioni 7.

“Kwa kipindi cha miaka miwili ijayo tunapanga kuwekeza kweye miundombinu ya mtandao kwa kuiboresha zaidi, kuongeza ubora wa huduma na kupanua wigo wetu ili kukidhi mahitaji ya jamii kwani dunia inahitaji huduma za kidijitali.

Eneo lingine tutakalowekea mkazo ni kuongeza wateja wa Halopesa kufukia milioni tano ambapo kwa sasa tuna idadi ya wateja zaidi ya milioni 2.4,” amesema Salum.

Ameongeza kuwa Halotel tayari imezindua huduma ya 4G katika maeneo mengi hapa nchini na imejenga vituo vya kusambazia huduma hiyo katika maeneo mengi ambapo idadi ya vituo hivyo kwa sasa ni mara mbili zaidi ya idadi iliyokuwa awali ikiwa wateja wanaotumia laini za 3G kwa sasa wanaweza kubadili laini zao kuwa za 4G bila malipo.

”Kwa huduma ya 4G , wateja wanaotumia huduma ya 3G wanaweza kubadili laini zao za 3G kuwa za 4G bila malipo na watapata ofa ya intaneti ya GB4 bure za kutumia kwa mda wa siku tatu.

“Katika kusherehekea miaka sita na kuhakikisha kuwa huduma inawafikia watu wengi, tungependa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuchagua mtandao wa Halotel kwa kipindi chote hicho na leo tunawazawadia wateja wetu kupitia kampeni maalumu inayojulikana kama ‘Recharge promotion’ kupitia kampeni hii mteja atapata asilimia 20 zaidi ya salio atakaloongeza ambapo promosheni hii ni kuanzia leo tarehe 15 Oktoba hadi tarehe 16 mwezi huu,” amsema.

Aidha HaloPesa chini ya Halotel inasherehekea miaka mitano ya kutoa huduma ya bora za kifedha, katika kusherehekea huko, inapenda kutoa shukrani kwa wateja kwa kuwapa promosheni ya kurudisha asilimia 100 ya makato ya mteja atakayokatwa na HaloPesa akituma pesa kwenda Halotel na anapo nunua luku kuanzia Oktoba 15 hadi 16, 2021.

Amesema kuwa mpango mwingine ni kuwekeza zaidi katika kutoa huduma ya kiteknolojia ya habari na Mawasiliano (Tehama), ili kuwafanya watumiaji wa simu janja kuweza kuperuzi katika mitandao sambamba na kuweza kunufaika kutokana na mahitaji yao katika kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha, kampuni ya Halotel ni Tawi la Kampuni ya Kivietnam Viettel Group ya nchini Vietnam amabayo ilianza kuitoa huduma zake hapa nchini mnamo mwaka Oktoba mwaka 2015 kwa kujikita zaidi katika kupeleka hudum za mawasiliano kwa watu waishio vjijini na hivyo kufanyan kampuni hiyo kufikia asilimia 95 ya Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles