26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

MAKUSANYO YA JIJI DAR YAZIDI KUPAA

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita

NA CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amesema mfumo wa mashine za kielektroniki (EFD), hasa katika maegesho ya magari, umesaidia jiji kukusanya mapato yanayofikia Sh bilioni 1.5 kwa mwezi kutoka milioni 500 za awali.

Akizungumza na MTANZANIA jana Dar es Salaam, Meya Mwita alisema katika makusanyo hayo, awali walikuwa wakikusanya Sh milioni 380 hadi 420  kwa makusanyo ya stakabadhi, huku fedha nyingine zikiishia katika mikono ya wajanja.

“Tunashukuru mfumo wa EFD umesaidia ongezeko la mapato ya zaidi ya Sh milioni 500, walau sasa baada ya muda fulani tunaweza kufanya jambo la maendeleo tofauti na hapo awali.

“Kwa sasa jiji limegawa mashine katika wilaya zote, ambazo zitatumika kukusanya mapato ya maegesho na ninawaomba wananchi wote pindi wanapofanya malipo ya maegesho ya magari yao, wasilipe fedha na kupewa stakabadhi za makaratasi.

“Kuanzia sasa nimekwisha tangaza ni bora mtu asilipe ushuru endapo atakutana na mkusanyaji anayetumia mfumo wa risiti,” alisema Meya Mwita.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jiji ili waweze kuendelea kuimarisha miundombinu na kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles