26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

DK. SENKORO KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI

Dk. Anna Senkoro
Dk. Anna Senkoro

Na FRANK SHIJA- MAELEZO

MWILI wa aliyekuwa mgombea wa kwanza mwanamke kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Anna Senkoro, unatarajiwa kuzikwa  kesho katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, msemaji wa familia, Fred Sendim, alisema mipango ya mazishi inakwenda vizuri.

“Mipango ya mazishi inaendelea vizuri nyumbani kwake Segerea, pia nitumie fursa hii kutoa shukrani za kipekee kwa wote wanaoendelea kutufariji na kushirikiana nasi bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu,” alisema Sendim.

Alisema kuwa taratibu za mazishi zitatanguliwa na ibada maalumu itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho kuanzia saa saba mchana katika Kanisa la Winners lililopo Banana, Ukonga, jirani na kituo cha mafuta cha Oil Com.

Sendim alisema Dk. Senkoro alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na juzi saa 11 alfajiri alizidiwa na kupelekwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa matibabu na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alifikwa na mauti.

Dk. Senkoro aliyegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kupitia Chama cha APPT-Maendeleo, ameacha watoto watatu na wajukuu wawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles