29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda atoa Sadaka zaidi ya misikiti 1,000

Brighiter Masaki.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Paul Makonda amewakabidhi shehena ya viungo vya kutengeneza futari kwa maimamu, mashehe na viongozi wa Dini ya Kislamu kutoka Misikiti zaidi ya 1,000 kama sehemu ya sadaka na shukrani ya Amani na Utulivu ndani ya mkoa huo.

Amekabidhi vitu hivyo leo Mei 20 Jijini Dar es Salaam,ikiwa pamoja na Mchele, Sukari, Unga, Maharage, Mafuta na vitu mbalimbali kwaajili ya kuwawezesha viongozi hao kufurahia futari majumbani mwao.

“Napenda kutoa shukrani zangu kwa uongozi wa dini kwa kuwa wasimamizi wazuri wa Amani na mshikamano ndani ya mkoa huu jambo linalofanya mkoa kuendelea kuwa kisima cha Amani”,amesema Makonda.

Aidha amesema Viongozi wa Dini kuwa namna bora ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli na kumuombea ni kuhakikisha waumini wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wachague viongozi wa serikali za mitaa wanaochukia Rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles